Issa Hayatou apigwa faini na mahakama ya kiuchumi ya Misri

issa Hayatou apigwa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Issa Hayatou, rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) na and Hicham El Amrani, ambaye alikuwa katibu mkuu wa zamani wa shirikisho hilo

Issa Hayatou, rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) na Hicham El Amrani, ambaye alikuwa katibu mkuu wa zamani wa shirikisho hilo wamepigwa faini ya dola za kimarekani 27.9m kila mmoja na Mahakama ya kiuchumi ya Misri kwa kukiuka sheria za nchi hiyo .

Mahakama hiyo ya kiuchumi iliamua kwamba wawili hao walikiuka sheria za Misri wakati wa kusaini mkataba wa dola za kimarekani bilioni 1 baina ya Caf na vyombo vya habari vya Kifaransa Lagardere mnamo mwaka 2015.

Hayatou alikuwa raisi wa shirikisho hilo tangu mwaka 1988 hadi mwaka jana, na El Amrani, ambaye pia alijiuzuru nafasi yake mwaka jana kwa pamoja wameamua kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama hiyo ya kiuchumi nchini Misri.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii