Mzozo wa Ukraine na Urusi: Merkel ailaumu Urusi kwa uchokozi

Angela Merkel amesema 'ni majadiliano tu' yatasuluhisha mzozo huu Haki miliki ya picha ACTION PRESS/REX/SHUTTERSTOCK
Image caption Angela Merkel amesema 'ni majadiliano tu' yatasuluhisha mzozo huu

Kansela wa Ujeremuni Angela Merkel amesisitiza kuwa hakuna suluhisho lolote la kijeshi katika mzozo wa majini kati ya Ukraine na Urusi katika pwani ya Crimea.

Jumapili iliyopita, wanajeshi wa Urusi ilipiga risasi manuari tatu za Ukraine ambazo zilikuwa safarni kuelekea kwenye lango la bahari ya Azov, na kuwakamata wafanyakazi wa manuari hizo.

Bi Merkel ameilaumu Urusi kwa mzozo huo, lakini akasema kwamba unaweza kutatuliwa kupitia "majadiliano ya wazi".

Merkel amezungumza hayo akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Ukraine, Volodymyr Groysman kwenye kongamano la kibiashara lililofanyika mjini Berlin.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemlaumu mwenzake wa Ukraine Poroshenko kwa kuanzisha uchokozi ili kujipatia umaarufu kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2019.

Awali Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameiomba Nato kutuma meli kwenda bahari ya Azov kufuatia makabiliano yaliyotokea kati ya Ukraine na Urusi baharini eneo la Crimea.

Poroshenko aliliambia gazeti la Ujerumani Bild kuwa anaamini kuwa meli hizo zitapelekwa "kuisaidia Ukraine na kuweka ulinzi".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanajeshi wa Ukraine kwenye bandari ya Mariupol bahari ya Azov

Siku ya Jumapili Urusi ilivamia meli tatu za Ukraine na kuwashika mabaharia wake kutoka Kerch strait.

Nato imesema inaunga mkono Ukraine ambayo si mwanachama wake.

Siku wa Jumatano Rais wa Urusi Vladimir Putin alimlaumu Bw Poroshenko kwa kuanzisha uhasama wa baharini ili kujiongeze umaarufu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019.

Rais Poroshenko alitanga sheria ya kijeshi sehemu za mpaka wa Ukraine kwa siku 30 kama jibu kwa mzozo huo.

Poroshenko alisema nini?

Wakati wa mahojiano na Bild, Bw Poroshenko alisema Vladimir Putin alikuwa na mpango wa kudhibiti bahari ya Azov.

"Ujerumani ni mmoja wa washirika wetu wa karibu sana na tunamatumaini kuwa nchi kwenye Jumuiya ya Nato sasa ziko tayari kupeleka meli katika bahari ya Azov ilia kuisaidia Ukraine kuweka ulinzi," alisema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Poroshenko akiongea na wanajehi huko Chernihiv, kaskazini mwa Ukraine

"Hatuwezi kukubali sheria hii ya uchokozi ya Urusi. Kwanza ilikuwa ni Crimea, kisha mashariki mwa Ukraine, na sasa anataka bahari ya Azov. Ujerumani pia inastahili kujiuliza: Ni kipi tena Putin atafanya kama hatuwezi kumzuia?"

Siku ya Jumatatu, mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alitoa wito kwa Urusi kuziachilia meli za Ukraine na kusema ni lazima Urusi ijue kuwa kuna madhara kwa vitendo vyake.

Alisema kuwa Nato itandelea kutoa msaada kwa Ukraine ambayo ni mshirika wa Nato, ingawa si mwanachama kamili.

Nato haikujibu mara moja taarifa za hivi punde kutoka kwa Bw Poroshenko.

Kipi kilifanyika huko Crimea?

Takriban wanajeshi watatu wa Ukraine walijeruhiwa wakati walinzi wa mpaka wa Urusi walifyatulia risasi boti mbili za kivita za Ukraine na boti nyingine ndogo karibu na Crimea.

Rasi hiyo ilimegwa kutoka Ukraine na Urusi mwaka 2014.

Image caption Njia ya mashua za Ukraine tarehe 24 Novemba

Boti hizo za jeshi la wanamaji zilikuwa safarini kutoka Odessa kwenda Mariupol, bandari ya Ukraine iliyo bahari ya Azov wakati zilikabiliwa na meli za walinzi wa mpakani wa Urusi.

Nchi zote zilikubalina kutumia kwa pamoja bahari mwaka 2003 lakini uamuzi wa Urusi kufungua daraja katia eneo la Kerch Strait mwaka huu imeibua msukosuko.

Ukraine inasema Urusi inafunga makusudi Mariupol na bandari nyingi ya Berdyansk kuzuia meli kupitia Kerch Strait.

Mabaharia 24 wa Ukraine walikamatwa na sasa wamepewa kufungo cha miezi miwili na mahakama huko Crimea.

Putin alisema nini?

"Bila ya shaka huu ni uchokozi," rais wa Urusi alisema, akiongeza kwa "hii imepangwa na mamlaka za Ukraine. Na ninafikiria ni rais wa sasa kabla ya uchaguzi wa urais nchini Ukraine Machi mwaka 2019".

Bw Poroshenko ana umaarufu mdogo. Kura za maoni za hivi majuzi zilionyesha kuwa ni asilimia 10 ya wapiga kura wanaopanga kumpigia kura mwaka ujao huku karibu asilimia 50 wakisema hawatampigia kura kwa vyovyote vile.

Alisisitiza kuwa jibu la jeshi la Urusi lilihitajika kwa kuwa Ukraine ilikuwa imevuka na kuinga maji ya Urusi.

Majibu mengine yamekuwa ya aina gani?

Serikali za magharibi zimeunga mkono serikali ya Ukraine.

Siku ya Jumatano EU ililaani vikali vitendo vya Urusi lakini ikashindwa kukubaliana na vikwazo vipya dhidi ya Urusi.

Ilitoa wito kwa Urusi kuachilia meli hizo na mabaharia wake na kuheshimu uhuru wa Ukraine. Poland ilikuwa inataka vikwazo vipya dhidi ya Urusi huku Ujerumani na Ufaransa wakita misukosuko kutulizwa.

Image caption Maeneo yaliyo chini ya sheria ya jeshi Ukraine

Mada zinazohusiana