Klabu ya Ballybrack FC ilitangaza kimakosa kuwa mchezaji wake Fernando LaFuente amefariki

Bendera ya kona uwanjani Haki miliki ya picha Getty Images

Fernando LaFuente anasema amekuwa "akitazama kifo chake mwenyewe" baaada ya klabu aliyokuwa akiichezea kuripoti kuwa amefariki.

Wakati Ballybrack FC ilipoifahamisha ligi ya wakuu ya Leinster kwamba LaFuente amefariki katika ajali ya barabarani,moja ya mechi yao iliahirishwa na zile zilizofuata wakawa wanakaa kimya kwa dakika moja ili kutoa heshima mchezaji wao aliyefariki.

Klabu hiyo imeomba msamaha na wasimamizi wa ligi hiyo wameanza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

"Nilianza kutumiwa barua pepe kazini zilizo na ujumbe wa taarifa za kifo changu - hivyo ndivyo nilivyogundua kuwa nimekufa," LaFuente aliiambia RTE Radio.

Mhispania huyo ambaye alihamia Galway anasema klabu yake ya Ballybrack iliwasiliana naye wiki iliyopita na kumfahamisha kuwa huenda akakumbana na taarifa kwamba alihusika katika ajali.

Aliongezea kusema : "Nilijua kutakuwa na habari kunihusu lakini nilifikiria itakuwa kitu kama kuvunjika mguu au kitu kingine.

"Nilikuwa nyumbani jana baada ya kazi. nilikuwa nacheza mchezo wa video. Wakaniambia: 'Umekuwa mtu mashuhuri.'

"Ni kwa sababu nilikuwa nimevunjika mguu, nilijiambia hivyo. Sikujali kuwa sitashiriki tena mchezo wa kandanda. Sina tatizo lolote kwanini inipatie usumbufu wa kiakili? Wajua huu uwongo ambao hujia kila mtu akilini mara kwa mara."

LaFuente alikubaliana na wazo la mtu aliye katika miaka yake ya 20 "ambaye natazamia maisha ya siku za usoni" bila shaka kufa katika ajali ya barabarani ilikuwa jambo "kuhuzunisha" Lakini: "kwangu ilikuwa kitu cha kuchekesha kwasababu nimekuwa nikitazama taarifa za kifo changu mwenyewe."

Mchezo wa Ballybrack dhidi ya Arklow Town uliahirishwa kufuatia tangazo lao, na wasimamizi wa ligi wakatoa rasmi tangazo la kifo changu katika gazeti la Ireland ikifuatiwa na " salamu za rambi rambi" kwa familia na klabu yangu.

Haki miliki ya picha BBC Sport

Klabu ilisema "ilielezea kusikitishwa kwake na kosa lililofanywa na mmoja wa maafisa wake wa ngazi ya juu ".

Iliongeza kuwa "Kosa kama hilo ambalo kamwe halitakubaliwa limefanywa na mtu ambaye anakabiliwa na hali ngumu ya kibinafsi ambayo pia imeathiri washirika wa klabu nzima".

LaFuente alisema: "Nimejenga uhusiano mzuri na wao. Punde tu baada ya kupata habari hizi niliwaandikia.

Walinijibu moja kwa moja na wakakubali ukweli kuwa tangazo hilo linaendelea japo waliomba msamaha.

"Ilibidi nimpigie simu mama yangu haraka iwezekanavyo na cha kushangaza hakuwa na habari kuhusiana na kisa hicho. Aliona asubuhi ya leo picha yangu katika magazeti. Bado sijasema nae kwasababu hakujibu ujumbe wowote niliyomtumia."

Mwenyekiti wa ligi David Moran ameiambia radio ya RTE kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo amejiuzulu siku ya Jumanne.

LaFuente alisema hafikirii kwamba klabu ya Ballybrack ilikuwa "inaogopa" kucheza na Arklow.

"Nadhani walikuwa na wakati mgumu kupata wachezaji,"alisema.

"Hawachezi kandanda kitaalamu. Wengi wao wana kazi za muda na baadhi yao wanafanya kazi nchini Uingereza. Nadhani hiyo ndiyo tatizo. Haikuwa suala kubwa."

Ligi imeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na "itachukua hatua kwa mujibu wa sheria zao za ndani".

Haki miliki ya picha Liffey Wanderers
Image caption Wachezaji wa Liffey Wanderers wakisimama kimya kutoa heshima kwa LaFuente

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii