Muziki wa Reggae kutunzwa kama urithi wa utamaduni usioonekana

Bob Marley Haki miliki ya picha Mike Prior
Image caption Umaarufu wa Bob Marley unaendelea kushamiri miaka 37 baada ya kifo chake

Muziki wa Reggae umewekwa katika orodha ya kumbu kumbu ya utamaduni ambao unastahili kulutuzwa kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa.

Muziki huo ambao chimbuko lake ni Jamaica ulianza miaka ya 1960 kutokana na juhudi ya wasanii kama vile Toots na the Maytals, Peter Tosh na Bob Marley, umeongezwa katika orodha hiyo kutokana "urithi wa utamaduni usioonekana".

Shirika la umoja wa mataifa la Sayansi, elimu na utamaduni Unesco, linasema Reggae "inawajenga wafuasi wake kimawazo, kijamii, kisiasa, na kiroho".

Muziki huu "umepenya kila pembe ya dunia,"ameongeza msemaji wa Jamaica.

Reggae imetokea eneo la Caribbean miaka ya 1960, na kujiimarisha kama mtindo wa kivyake kutokana na mitindo ya muziki wa ska na rocksteady, ambao waanzilishi wake wa wali kama vile Lee Scratch Perry, Prince Buster na Wailers, walitambuliwa na Marley, Tosh na Bunny Wailer.

Muziki wa Reggae ulikuwa maarufu sana nchini Marekani lllllakini uliimarika zaidi Uingereza.

Hii ni kwasababu Uingereza ilikuwa nyumbani kwa wahamiaji wengi kutoka Jamaica tangu mwishowa vita vikuu vya pili vya Dunia.

Mwaka jana Jamaica ilikuwa imetoa maombi ya kutaka muziki huo kujumuishwa katika orodha ya ya Unesco wakati alipokuwa na mkutano katika kisiwa cha Mauritius

Shughuli ya kulinda orodha ya urithi wa utamaduni usioonekana ilianza mwaka 2008 na ilitokana na azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2003.

Lengo la azimio hilo ni kuhakikisha jamii zinaheshimika pamoja na makundi na watu waliyoorodheshwa katika shughuli za kulinda na kuimaridsha utamaduni Kitaifa na Kimataifa.

"Reggae inahusishwa sana na Jamaica,"alisema waziri wa utamaduni wa Jamaica Olive Grange "Ni muziki ambao tumeukuza sisi na umepenya kila kona ya dunia."

Ikitaoa uamuzi huo ,Unesco (Shirika la Umoja wa Mataifa la kusimamia elimu sayansi na utamaduni) ilisema maudhui ya muziki huo "imechangia utangamano wa kimataifa kwa kuangazia masuala ya haki, upendo na umoja".

Utamaduni mwengine uliyoshirikishwa katika orodha hiyo ni kuendesha baisikeli kuenda shuleni mjini Vienna, Utamaduni wa Mongolia wa kumbembeleza ngamia na utamaduni wa vikaragosi nchini Czech.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii