UN:Ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binaadamu

uchafuzi wa hali ya hewa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Viwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa

Umoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani.

Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

Mkutano umeanza rasmi mapema Jumatatu, ni mkutano mkubwa wa hali ya hewa na tabia nchi kufanyika tangu ule wa Paris wa mwaka 2015.

Wakati huo huo Benki ya dunia, imetoa dola bilioni 200 zilizoelekezwa kwa nchi zinazochukua hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka mitano ijayo.

Rais wa umoja wa mataifa katika masuala ya hali ya hewa, Maria Esposa amesema kuwa jitihada za haraka zinahitajika.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Athari za mabadiliko ya hali ya hewa

''Tulipoanza na mkutano wa masuala ya hali ya hewa mwaka 1995, ni kama tulikua tukipanga maisha ya baadae, na tulikua tukizuia kuharibika kwa hali ya hewa, lakini sasa tunaishi ndani yake, sasa tunatakiwa tujikomboe haraka , na jamii inatakiwa ikubaliane na mabadiliko haya.

Esponsa, amesema pia wajumbe wamekutana ili kujadili namna ya kujikomboa na mabadiliko hayo ya tabia nchi, na kuhakikisha makubaliano ya Paris yanafanyiwa kazi.

Viongozi wanne wa umoja wa mataifa waliomaliza muda wao, na wazungumzaji wakuu kuhusu hali ya mabadiliko ya tabia nchi, walitoa tamko la kutaka jitihada za haraka kuchukuliwa ili kuzuia mabadiliko haya ya kasi.

Haki miliki ya picha SOPA IMAGES

Wamesema kuwa hatua ndani ya miaka miwili zinaweza kupunguza janga hili.

Ombi la mwisho kuepusha 'janga la hali ya hewa'

Wakati huohuo nchi kadhaa zimekua zikitoa tamko juu ya kuhakikisha wanapambana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini hatua wanazochukua haziridhishi.

Kutokana na suala hili kuwa la dharura, baadhi wa wadau walikutana mapema jana kujadili kabla kikao hakijaanza rasmi.

Viongozi wa nchi 29 wanatarajiwa kuhudhuria , kwa upande wa China na Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuonyesha kuwa kuna uwezekano wa ushirikiano wa pamoja hata katika kipindi hiki cha uongozi wa Donald Trump nchini Marekani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii