Uchaguzi 2020: Hapa Kazi Tu vs Kazi na Bata, Bernard Membe 'kutaka' urais vyakoleza joto la siasa Tanzania

Magufuli na Lowassa
Maelezo ya picha,

Rais John Magufuli alimshinda Edward Lowassa katika uchaguzi mkuu wa 2015

Tanzania inatarajiwa kuenda kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020, lakini tayari joto la uchaguzi huo limeanza kupanda.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa chama tawala cha CCM Dk Bashiru Ally alikuwa kiongozi wa kwanza mkubwa wa CCM kuonesha dalili ya kupanda kwa joto hilo.

Kiongozi huyo alidai kuwa amekuwa akisikia taarifa kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe amekuwa akipanga kimya kimya mikakati ya kugombea urais ifikapo 2020.

CCM wamekuwa na utaratibu wa kumpitisha bila kupingwa rais aliyemaliza muhula wake wa kwanza wa miaka mitano, kuchukua tiketi ya kugombea urais tena kwa miaka mitano ya mwisho kikatiba bila kupingwa.

Rais aliye madarakani kwa sasa, John Magufuli atamaliza muhula wake wa kwanza 2020 na atarajiwa kuomba tena ridhaa ya chama chake kuwania urais kwa miaka mitano mingine.

Membe aligombea tiketi ya CCM 2015 na kuchujwa katika vikao vya ndani ambapo hatimaye Magufuli kupewa ridhaa. Toka wakati huo, amekuwa kimya na kutojishughulisha na masuala ya kisiasa.

Hata hivyo, Dk Bashiru anasema kumekuwa na taarifa kuwa Membe anajipanga kumkwamisha Magufuli ifikapo 2020.

"Kati ya wagombea wote wa CCM ni Membe peke yake ambaye sijakutana naye, namkaribisha ofisini, aje anieleze ninayoyasikia ni kweli au si kweli."

"Kwani haya yanayozungumzwa nyie hamyasikii? nasema peke yangu? Mimi ndiyo katibu mkuu wa CCM aje ajitetee kwamba yeye si kikwazo," alisema Dk Bashiru

"Iweje watu waseme kwamba wewe (Membe) unafanya vikao vya kutafuta kura za 2020, kwamba unataka kumkomesha Rais Magufuli, halafu unakaa kimya tu? sasa mimi nakualika uje ofisini…"

Baada ya kauli hiyo ya Dkt Bashiru, kulitambaa ujumbe kwenye mitandao unaodaiwa kutoka kwa Membe akishangaa namna iliyotumika kumuita lakini akaahidi kuitikia wito atakaporejea nchini.

Katika ujumbe huo, 'Membe' alitaka aliyeanzisha tuhuma hizo dhidi yake pia awepo ili athibitishe. Hata hivyo, Dkt Bashiru alijibu mapigo na kusema hawezi kuwekewa masharti na mwananchama wa 'kawaida'.

Sakata hilo la Mmembe limezua mjadala mkubwa mitandaoni. Rais wa Chama cha Wansheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume alihoji iwapo kutaka kugombea urais kwa Membe ni kosa.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Watumiaji wengine wa mtandao wakenda mbali na kuanza kumpigia chapuo Membe kuwa wanaimani kubwa kwake ifikapo 2020.

Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Ruka Twitter ujumbe, 3

Mwisho wa Twitter ujumbe, 3

Ila wapo ambao wameonya kuwa kupigiwa huko chapuo kunaweza kusababisha Membe kuvuliwa uanachama wa CCM.

Ruka Twitter ujumbe, 4

Mwisho wa Twitter ujumbe, 4

Kazi na Bata

Katika hatua nyengine, Kiongozi wa chama cha upinzani Zitto Kabwe ameunda kauli mbiu mpya kwa ajili ya siasa za uchaguzi wa 2020, Kazi na Bata. Kauli mbiu hiyo, ni kinyume cha ile ya Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Kula bata, kwa lugha ya mtaani nchini Tanzania inamaanisha kustarehe. Hivyo, kauli hiyo inalenga kuhamasisha kazi lakini pia na mapumziko na starehe.

Ruka Twitter ujumbe, 5

Mwisho wa Twitter ujumbe, 5

Zitto pia ametumia upepo wa Membe, akisema hata ikiwa ni yeye ndiye atatwaa urais ifikapo 2020 basi kauli mbiu hiyo asiitupe. Pia akamtaja Tundu Lissu ambaye anatajwa kutaka kuwania urais kupitia Chadema. Lissu bado yupo Ubelgiji akipata matibabu baada ya kushambuliwa na risasi mwaka jana. Na mwisho akamtaja na Edward Lowassa (ama mzee Edo).

Ruka Twitter ujumbe, 6

Mwisho wa Twitter ujumbe, 6

Kauli mbiu hiyo tayari imezua gumzo na wapo wanaojiuliza kama itaweza kuwahamasisha vijana kuunga mkono upinzani ifikapo 2020.

Ruka Twitter ujumbe, 7

Mwisho wa Twitter ujumbe, 7

Lakini wapo ambao wanaamini kauli hiyo inachochea uzembe, na kutaka kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu iendelee kuenziwa kivitendo.