Michelle Obama aelezea hofu ya muda mrefu, anasema wakati mwingine uhisi kukosa kujiamini

Michelle Obama at the Royal Festival Hall Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michelle Obama huku Royal Festival Hall

Michelle Obama amesema kuwa bado huwa anaingiwa na woga na kujawa na shaka ndani ya nafsi yake, kitu ambacho amejaribu kukitokomeza bila mafanikio.

Bi Obama alikuwa akizungumza wakati alirudi huko Elizabeth Garrett Anderson School, kaskazini mwa London ambapo alikuwa amezuru mwaka 2009.

Mke huyo wa zamani wa rais wa Marekani alihudhuria warsha moja katika ukumbi wa Royal Festival mjini London.

Akiwa hapo alikumbuka jinsi malkia alivunja mipangilio na itifaki wakati yeye na Rais Obama walizuru makao ya kifalme ya Windsor Castle.

Anasema alikuwa na hofu kuhusu mienendo yake mbele ya malkia lakini Malkia alisema: "Ingia tu" .

Jana Jumatatu Bi Obama alifanya mazungumzo na mwandishi vitabu Chimamanda Ngozi Adichie kukipigia debe kitabu chake kipya chenye kichwa Becoming.

Zaidi ya watu 40,000 walijaribu kupata kununua tikiti kwa njia ya mtandao wakati hafla hiyo ilitangazwa.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mrs Obama was in conversation with Nigerian author Chimamanda Ngozi Adichie

Na mwezi uliopita kitabu hicho chake kilichukua nafasi ya kwanza kilichouzwa zaidi mwaka huu siku 15 tu baada ya kuchapishwa.

Bi Obama alihutubia wanafunzi 300 wa shule ya Elizabeth Garrett Anderson huko Islington kama sehemu ya ziara yake.

Alizuru kwa shule hiyo wakati wa mkutano wa G-20 miaka 9 iliyopita miezi michache baada ya kuwa mke rais.

Alipoulizwa jinsi alihisi kwa kuonekana kama "mfano wa matumaini", Bi Obama aliwaambia wanafunzi kuwa hisia ya kukosa kujiamini, haiendi, kuwa kweli mnanisikiliza.

Haitoki kuwa hamstahili kunitilia maanani. Ni kitu gani ninajua? Ninawaambia haya yote kwa sababu sote tuna shaka kuhusu uwezo wetu, kuhusu nguvu zetu na nguvu hizo ni zipi.

Kama ninawapa watu matumaini huo ni wajibu, kwa hivyo ni lazima nihakikishe kuwa nimejibika.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Hatuna namna nyingine lakini kuhakisha sisi wakubwa tunawapa vijana sababu ya kuwa na matumaini."

Bw Obama alihudumu mihula miwili huko White House. Bi Obama ni wakili na ameongoza mashirika kadhaa likiwemo la Let Girls Learn, kuunga mkono elimu kwa wasichana kote duniani.

Hekima yake kwa wanawake wachanga?

"Ushauri wangu kwa wanawake wachanga ni kwanza kutoa zile imani mbaya kutoka vichwa vyao. Swali ninalojiuliza mimi - mimi ni mzuri? - hili hutusumbua sisi kwa sababu ujumbe unaotumwa tangu tuwe wadogo ni kuwa usifike mbali sana usiongee kwa sauti sana."

Hii ndiyo siri," aliongeza. "Nimekuwa kwa kila meza ya juu ambayo unaweza kuifikiria, nemefanya kazi na mashirika yasiyo ya serikali, nimekuwa kwenye wakfu, nimefanya kazi kwenye makampuni, kwenye bodi za kampuni, nimekuwa kwenye mikutano ya dunia, nimefanya kazi UN: wao sio werevu sana

Mada zinazohusiana