Wanariadha wa Urusi kuendelea kuitumikia adhabu iliyotolewa na shirikisho la riadha duniani IAAF

Sebastian Coe na Rune Andersen Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rune Andersen (kulia), akiwa na Rais wa IAAF, Sebastian Coe, amesema IAAF haina uhakika kama itapokea sampuli kutoka kwenye Maabara ya Moscow

Wanariadha wa Urusi wataendelea kuzuiwa kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya shirikisho la riadha duniani, IAAF kusogeza mbele adhabu mpaka mwaka 2019.

Shirikisho hilo liliipiga marufuku Urusi mwezi Novemba mwaka 2015 baada ya ushahidi kuwa nchi hiyo ilidhamini wanariadha wake kufanya udanganyifu.

Marufuku hiyo itaendelea kuwepo mpaka sampuli na data kutoka maabara ya mjini Moscow zitakapopatikana.

Urusi pia inalazimika kulipa gharama zote ziizotumiwa na kikosi kazi cha IAAF.

''Nina matumaini watatoa majibu ya Data mwishoni mwa mwaka huu,'' alieleza Rune Andersen, Kiongozi wa kikosi kazi cha IAAF kilichokuwa kikifanya uchunguzi Urudi

alisema ''siwezi kwenda mbali zaidi, hatujapokea uthibitisho wowote kuwa ushahidi utatufikia moja kwa moja.''

Haki miliki ya picha AFP

''Shirika linalopiga marufuku matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni, (WADA) lilihakikishiwa kuhusu hilo, na WADA waliwapa mpaka tarehe 31 mwezi Desemba wawe wameshapokea Data.

''Tunategemea Data ambazo itapatiwa WADA kabla ya kuzikisha kwa kikosi cha AIU''.

Hii ni mara tisa kwa kwa IAAF kukataa rufaa ya Urusi.

Mwezi Februari Urusi ilirudishiwa uanachama wake wa Olimpiki baada ya kufungiwa wakati wa michuano ya pyeongchang majira ya baridi mwaka 2018.

Hata hivyo Wada iliwafungulia mwezi Septemba baada ya kuizuia kwa miaka mitatu.

Hatua hii inamaanisha kuwa wanariadha hawataweza kushiriki kwenye mashindano ya ndani ya Ulaya mwezi Februari.

Hata hivyo wanariadha walipita vipimo wataruhusiwa kushiriki kibinafsi bila bendera ya Urusi katika mashindao ya riadha ya mataifa ya Ulaya ya uwanja wa ndani mjini Glasgow mwezi Februari mwakani.

Wakati huo huo IAAF imetangaza kuwa mbio za dunia za mwaka 2023 zitafanyika mjini Budapest, Hungary.

Mada zinazohusiana