Mazishi ya George HW Bush: Viongozi watoa heshima zao

Members of the public pay their respects to former US President George H.W. Bush at the Rotunda of the US Capitol in Washington, DC, USA, 04 December 2018 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wakitoa heshima zao kwa rais wa zamani George H.W. Bush

Viongozi wa dunia na wageni mashuhuri wamewasili nchini Marekani kutoa heshima zao wakati wa mazishi ya rais wa zamani wa Marekani George HW Bush.

Mwili wa Bush ambao umekuwa kwenye bunge la Marekani, umehamishwa kwenda kanisa kuu la National Cathedral huko Washington kwa mazishi.

Mtoto wake, rais wa zamani George W Bush atatoa rambi rambi.

Bush senior, ambaye alihudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki Ijumaa akiwa na miaka 94.

Atazikwa nyumbani kwao huko Texas kando na kaburi la mke wake Barbara.

Kipi kitafanyika kwenye mazishi?

Mazishi hayo yamenza huko Washington DC.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Thousands of Americans have visited the Capitol Rotunda to say a final goodbye

Rais Donald Trump na mtangulizi wake Barack Obama, Bill Clinton na Jimmy Carter wamehudhuria misa hiyo.

Mwanaufalme wa Wales, Chansela wa Ujerumani Angela, Merkel na mfalme wa Jordan Abdullah II ni kati ya viongozi wa dunia ambao wanatoa heshima zao.

Viongozi wa zamani wakiwemo John Major, ambaye alihudumu kama waziri mkuu wa Uingereza wakati wa muhula wa Bush pia amehudhuria.

Leo Jumatano imetangazwa kuwa siku ya taifa ya kuomboleza na ofisi nyingi za serikali na soko la hisa la Marekani limefungwa.

Baada ya mazishi mwili wa Bush utasafirishwa kwenda Taxas ambapo utakaa kwa umma hadi Alhamisi asubuhi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa zamani George W. Bush na mke wake Laura wakitoa heshima zao

Kutakuwa na misa ya pili kabla ya Bush 4141 - treni iliyopewa jina kwa heshima ya rais huyo wa zamani kusafirisha mwili wake hadi eneo la kuzikwa katika maktaba ya rais ya George HW Bush.

George H W Bush alikuwa mtu wa aina gani?

Kuapishwa kwa George H W Bush kuwa Rais wa Marekani mnamo Januari 1989 kilikuwa kilele cha ufanisi wake katika siasa. Alikuwa ameandiliwa kwa muda mrefu kupitia mafunzo ya kiwango cha juu, na kupandishwa madaraka mara kwa mara kabla ya kuishia Ikulu ya White House.

Rais huyu wa 41 wa Marekani alifanya kazi kama makamu wa Rais wa Ronald Reagan kwa miaka minane.

Alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza aliyekuwa afisini kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais katika kipindi cha zaidi ya miaka 150.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption George H W Bush

Utawala wake unahusishwa sana na siasa za wakati ule ambapo Ukomunisti ulikuwa ukiporomoka Ulaya Mashariki na kusambaratika kwa Muungano wa Usovieti (USSR) ambapo Marekani iliachwa ikiwa taifa kubwa zaidi kiuchumi na kiviwanda duniani.

Uongozi wake ulisaidia kurejesha hadhi ya Marekani kwa dunia nzima na kurejesha heshima yake kufuatia uvamizi wa Marekani nchini Vietnam, ulioiletea Marekani aibu.

Hata hivyo alilaumiwa kwa kupuuza maswala ya ndani ya Marekani na kwa kupuuzilia mbali ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ambapo aliahidi kuwa hataongeza kodi.

Kupuuzilia mbali kwa ahadi hiyo kulimfanya ashindwe katika uchaguzi uliofuata na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1992.

Maisha ya kisiasa ya Bush Sr

  • 1966: Alishinda kiti katika Bunge la Wawakilishi
  • 1971: Nixon amteua kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa
  • 1974: Ateuliwa kuwa Balozi wa Marekani katika ubalozi mpya nchini Uchina
  • 1976: Ford amteua kuwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la CIA
  • 1981-1989: Makamu wa Rais wa Ronald Reagan
  • 1989-1993: Rais wa Marekani; aongoza Marekani katika Vita vya Kwanza vya Ghuba; akabiliana na hali ya kuporomoka kwa Ukomunisti Ulaya Mashariki.

Mbwa wa Bush Sully aliyegusa wengi kwa heshima zake za mwisho

Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.

Haki miliki ya picha OFFICE OF GEORGE HW BUSH
Image caption Picha ya kwanza ya Mbwa Sully akiwa amelala karibu na jeneza lenye mwili wa George HW Bush iliyowagusa wengi

Bw Bush, aliyehudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa na miaka 94.

Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, alisafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda Washington DC siku ya Jumatatu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sully alisafiri na Air Force One iliyoubeba mwili wa marehemu kwenda Washington Jumatatu

Mbwa huyo wa jina Sully alisindikiza jeneza hilo muda wote.

Picha ya kwanza kabisa ya Sully akitoa heshima zake ilipakiwa mtandaoni na msemaji wa Bw Bush Jim McGrath, pamoja na ujumbe: "Mission complete."

Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao.

Mada zinazohusiana