Sanamu ya shetani kuashiria msimu wa sherehe yawekwa kwenye jengo la serikali Illinois Marekani

Satanic statue in place at Illinois' statehouse Haki miliki ya picha Facebook/The Satanic Temple - Chicago Chapter
Image caption Sanamu ya shetani kwenye jengo la serikakali huko Illinois

Kundi la kishetani limeongeza sanamu yake kwenye sanamu zingine katika jengo moja la serikali jimbo la Illinois kuashiria msimu huu wa sherehe.

Ikiwa karibu na mti wa krismasi sanamu inaonyesha nyoka aliyejipinda kwanye mkono unaoshika tunda la tofaa

Ndiyo sanamu ya kwanza kuletwa na hekalu la shetani la chicago.

Serikali ya jimbo hilo ilisema kuwa hekalu hilo lika haki sawa na makundi mengine ya kidini kuweka sanamu yake eneo hilo.

Chini ya katiba watu wana haki ya kutoa hisia zao, na fikra zao kwa mujibu wa Dave Druker, msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa jimbo la Illinois.

Hatua hiyo imekosolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Hekalu la shetani ni nini?

Lilianzishwa mwaka 2012 huko salem, Massachusetts.

Linasema linatumia nembo za kishetani kuonyesha mgawanyiko kati ya kanisa na nchi na kupigia debe haki.

Lina mahekalu 15 kote nchini Marekani kubwa ziadi likiwa katika jimbo la Michigan.

Hekali hilo lilianzishwa na aliyekuwa mwanafanzi wa zamani wa chuo cha Harvard Doug Mesner au "Lucien Greaves", na mtu mwingine kwa jina "Malcolm Jerry".

Mapema mwaka huu wanachama wa hekalu hilo la shetani waliweka sanamu ya mbuzi inayohusiana na ushetani nje ya jengo moja ya serikali huko Arkansas.

Kundi hili pia liliafikia makubaliano ya dola milioni 50 kwenye kesi dhidi ya kampuni za Netflix na Warner Bros mwezi uliopita kuhusu sanamu iliyotumiwa kwenye filamu ya The Chilling Adventures of Sabrina.

Mada zinazohusiana