Putin: Urusi itatengeneza makombora iwapo Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo

Rais wa Urusi Vladimir Putin Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Putin anasema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba

Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo, ameonya rais Vladimir Putin.

Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri.

Rais wa Putin amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

Katika tamko hilo lililoangaziwa kwenye televisheni, kiongozi huyo alisema mataifa mengi yanaunda silaha zilizopigwa marufuku katika mkataba wa INF

"Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaonelea ni lazima wao pia wawe na silaha ," alisema.

"Jibu letu ni nini? Bila shaka - sisi pia tutafuata mkondo huo."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Donald Trump wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump siku za hivi karibuni aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba huo kutokana na mienendo ya Urusi.

Wadadisi wanasema Urusi unachukulia suala la uundaji wa silaha hizo kama mbinu mbadala ya kuimarisha vikosi vyake na gharama yake ni nafuu.

Alipowasili kwa mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa EU, Kiongozi wa muungano wa Ulaya anayesimamia sera za nje Federica Mogherini ametoa wito kwa mataifa hayo mawili kudumisha mkataba huo akiongeza kuwa "Umekuwa hakikisho la amani na usalama barani Ulaya kw amiaka 30 sasa".

Nato imesema nini?

Siku ya Jumanne, shirika la Nato liliikosoa rasmi Urusi kwa kukiuka kanuni zinazoongoza mkataba huo.

Katika taarifa shirika hilo lilisema: "Washirika wa wote wamekubaliana kuwa Urusi iliunda kombora aina ya ,9M729 ambayo inakiuka mkataba wa INF katika hatia ambayo inatishia usalama wa muungano wa Euro-Atlantic".

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa nchi wanachama wa muungano huo"zinaunga mkono" madai ya Marekani kwamba Urusi ilikiuka mkataba huo, na kuitaka Moscow "kuchukua jukumu la kuutekeleza kikamili".

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi

Akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesem,a Urusi ina siku 60 ya kurejelea makubaliano hayo ili kutoa nafasi kwa Marekani kusitisha utekelezaji wake.

"Katika kipindi hicho cha siku 60 hatutafanyia majaribio silaha zetu, kuunda au kutumia mfumo wowote , ili kuba nini kitakachofanyika katika kipindi hiyo" alisema.

Urusi imekuwa ikikanusha tuhuma za kukiuka mkataba wa vita baridi.

Ni yapi yaliyomo katika makubaliano ya kuunda makombora ya masafa ya kadri (INF)?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa Sovieti Mikhail Gorbachev na rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan walitia saini mkataba wa INF mwaka 1987
  • Mkataba huo uliotiwa saini na Marekani na USSR mwaka in 1987, ulikuwa wa kudhibiti uundaji wa silaha za nuklia na makombora ya masafa ya mafupi na ya kadri, isipokuwa yale ya kurushwa baharini.
  • Marekani ilikuwa na hofu kuhusiana hatua ya Usoviyeti kuunda kombora la USS-20 na kujibu hatua hiyo kwa kuunda makombora ya kulipua meli barani Ulaya - hatua hiyo ililaaniwa sana.
  • Kufikia mwaka 1991, karibu makombora 2,700 ilikuwa imeharibiwa.
  • Mataifa yote mawili yaliruhusiwa kukagua mitambo ya mwingine.
  • Mwaka 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin ilitangaza kuwa mkataba huo haulindi tena maslahi yake
  • Hatua hiyo ilikuja baada ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa mwaka 2002

Mwaka 2014,aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Barak Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa INF, kufuatia madai kuwa ilifanyia majaribio kombora lake la kulipua meli.

Obama aliripotiwa kudumisha mkataba huo kufuatia ushawishi kutoka kwa viongozi wa bra Ulaya, walisema hatua hiyo huenda akaanzisha tena mashindano ya uundaji silaha.

Mara ya mwisho Marekani ilijiondoa katika mkataba wa silaha ilikuwa mwaka 2002, wakati rais George W Bush alipojiondoa kutoka mkataba wa kudhibiti uundaji wa makombora ya nuklia ambayo ilipiga marufuku uundaji wa silaha za kujibu mahambulio ya silaha hizo.

Hatua ya utawala wake wa kuweka kituo cha kujikinga dhidi ya makombora barani ulaya iliikasirisha Kremlin.

Hata hivyo kituo hicho kilifungwa na utawala wa Obama mwaka 2009 na mahala pake pakachukuliwa na mfumo wa ulinzi uliyoimarishwa mwaka 2016.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii