Wanawake wanavyoadhibiwa kwa sababu ya makosa ya waume na ndugu zao Madagascar

Wanawake wanavyoadhibiwa kwa sababu ya makosa ya waume na ndugu zao Madagascar

Wanawake nchini Madagascar wanasema wamekuwa wakifungwa jela kwa makosa yaliyotendwa na jamaa zao wa kiume au hata waume zao.

BBC imezungumza na wanawake ambao wamezuiliwa gerezani kwa miezi, baadhi kwa miaka kadha.

Wanasema waliambiwa na maafisa kwamba wao ni "washirika" katika uhalifu au walifaa kufahamu makosa yaliyotendwa na waume zao, ndugu au wana wao wa kiume.

Makala hii ni sehemu ya msururu wa makala za Wanawake 100.