Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 08.12.2018: Lukaku, Hazard, Neymar, Mbappe, De Jong, Jimenez

Image caption Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku , 25 anaona kuwa hana siku nyingi katika timu ya Manchester United baada ya kukatishwa tamaa na Jose Mourinho. (Sun)

Mourinho anasema kwamba Manchester United haina nafasi ya kushinda ligi ya Premia hivi karibuni kama Manchester City na Liverpool wataendelea kusajili. (Mirror)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameanza jitihada za kumuwania kiungo wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27. (Standard)

Paris St-Germain walikuwa tayari kumuuza mshambuliaji kutoka Brazil Neymar, 26 au mchezaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 19, ili kuondoa vikwazo vya gharama za usajili.(L'Equipe - in French)Lakini PSG imekana taarifa na kulituhumu gazeti la L'Equipe kuwa kinyume na klabu yake. (PSG - in French)

Image caption Harry Maguire

Maneja wa Newcastle Rafael Benitez amekanusha dai la klabu hiyo kufanya mazungumzo ya awali ya kumsainisha kiungo raia wa Palaguay Miguel Almiron, 24, kwa dau la pauni milioni 15 akitokea ligi kuu ya Marekani ya klabu ya Atlanta United . (Goal)

Liverpool inajiandaa kumrejesha winga wake Harry Wilson, 21, aliyeenda kwa mkopo katika klabu ya derby inayoshiriki ligi daraja la kwanza ingawa majeraha yamekuwa tatizo kubwa kwa kinda huyo raia wa wales. (Liverpool Echo)

Kocha wa Arsenal Unai Emery imepinga adhabu kali wanayoelekeziwa wachezaji wanne wanaotuhumiwa kutumia dawa zinazosadikika kuongeza nguvu mwaka jana kabla ya msimu wa ligi kuanza. Unai anapinga kwa sababu ilikuwa kabla ligi kuanza. (Sun)

Winga wa West Ham na Scotland Robert Snodgrass amesema amerejea katika klabu yake akiwa amebadilika sana kutokana na ratiba ya chakula aliyokuwa nayo akiichezea Aston Villa msimu uliopita. (Mail)

Kiungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21 anataka kujiunga na PSG na sio Manchester City kipindi hiki cha kiangazi na upande wa Ufaransa wamejiandaa kulipa euro milioni 75 ili kusaini mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (De Telegraaf Dutch)

Manchester United na Chelsea wanamuwania mlinzi wa kushoto Alex Sandro ambaye ameripotiwa kusaini mkataba mpya na Juventus.Mchezaji huyo wa Brazil , 27 amejikita Turin mpaka 2023. (Sun)

Wolves watavunja rekodi kwa kulipa euro milioni 38 ili kumchukua mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez kutoka Benfica. (O Jogo - in Portuguese)

Meneja wa Leicester Claude Puel anatarajia mchezaji wa England Harry Maguire kubaki katika klabu hata kama Manchester United itatoa ofa nyingine ya kumsainisha mchezaji huyo mwezi Januari. (Sky Sports)

Mashetani wekundu Manchester United imeamua kumruhusu mshambulaiji wa klabu hiyo Alexis Sanchez kurejea Chile kuendelea na matibabu ya majeraha aliyoyapa akikitumikia kikosi hicho. (Independent)

Klabu ya Arsenal I imesema haitamrudisha mlinzi Callum Chambers, 23, anayeitumikia Fulham kwa mkopo hata kama nafasi ya ulinzi ya klabu hiyo inapata changamoto nyingi ikiwemo kuumia kwa kinda wao Rob Holding. (Evening Standard)

Klabu ya Manchester United inajiandaa kufanya usajili wa mshambuliaji kinda wa Bristol City Antoine Semenyo, 18, anayekipiga kwa mkopo Newport County. (Express)

Image caption Diego Costa

Atletico Madrid wamenuia kumsajili mashambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kuwa mbadala wa Diego Costa endapo atapata majeraha ya muda mrefu. (Marca)

Meneja wa klabu ya Brugge ya Ubeligiji Ivan Leko ameweka wazi kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Wesley Moraes, 22, ana uwezo wa kukipiga Arsenal ikifuatiwa na taarifa zilizotoka kuwa kinda huyo raia wa Brazil anahitajika na mabingwa hao wa London. (La Derniere Heure - in French)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameanza kumsajili na kuungana naye tena kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 23, (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mlinda lango wa Burnley Tom Heaton, 32, amekuwa kivutio kwenye dirisha dogo la usajili la januari kwa vilabu vya Aston Villa na Leeds. (Star)

Manchester United imefanikiwa kumubakiza kinda wake mwenye uraia wa Amienia Noam Emeran, baada ya vilabu vya Juventus, Valencia na PSG kuonyesha nia ya kumtaka. (RMC - in French)

Bosi wa Cardiff city Neil Warnock anafikiria kuwa sehemu nzuri yenye kufurahisha endapo atatimuliwa mwaka ujao(Januari), ameyasema hayo huku kukiwa na tetesi za kocha wa zamani wa Tottenham na QPR Harry Redknapp kuja kumrisi meneja huyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii