WHO: Idadi ya vijana wanaokufa kwa ajali za barabarani inazidi ya wanaokufa kwa virusi vya Ukimwi

ajali Haki miliki ya picha Getty Images

Ajali za barabarani zinatajwa kuwa ndio zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana duniani, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO).

Shirika hilo la afya limechapisha ripoti ambayo inabainisha kwamba bara la Afrika ndilo lina ajali nyingi za barabarani duniani.

Katika taarifa nyingi zinasema kwamba waafrika na wamarekani wa Kusini bado hawana sheria nzuri za kudhibiti mwendo kasi.

Lakini taarifa hizo zimesisitiza kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani duniani huwa zinalingana na kiwango cha idadi ya watu.

Ajali za magari ndio zinaongoza duniani kusababisha vifo kwa watoto na vijana wenye umri kati ya miaka mitano mpaka 29, ripoti hiyo imesema.

Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba watu wengi zaidi wanakufa kutokana na ajali za barabarani kuliko virusi vya ukimwi , kifua kikuu au magojwa ya kuhara.

"Vifo hivyo havikubaliki, hakuna sababu inayoweza kutetea matukio hayo .Hili ni tatizo ambalo linaweza kutafutiwa ufumbuzi" Mkurugenzi wa WHO alisema.

Ripoti ya Shirika la afya duniani inasema kwamba kuna vifo 27 kwa kila watu 1000 . Vifo vya barabarani katika nchi za Afrika ni mara tatu zaidi ya ajali zinazotokea Ulaya, ambako kuna ajali chache zaidi.

Imesema ni karibu nusu ya mataifa 54 ya Afrika hayana sheria za mwendo kasi katika nchi zao.

Botswana, Ivory Coast na Cameroon, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeona kiwango cha vifo vikiongezeka.

Egypt, Angola, Burkina Faso na Burundi ni miongoni mwa nchi ambazo wameshuhudia kuona ajali zikipungua.

Afrika ina kiwango kikubwa ya ajali ambazo zinasababisha vifo.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni , zinasema kuwa watu milioni 1.35 waliuwawa katika ajali za magari duniani kwa mwaka 2016, kiwango ambacho kiko tofauti kidogo na mwaka uliopita.

Hatari za ajali za barabarani katika nchi zinazoendelea ziko kiwango cha juu kwa mara tatu zaidi .

Kusini mashariki mwa bara la Asia inaongoza kuwa na ajali nyingi ikifuatiwa na Afrika pamoja na mashariki mwa Mediterania.

Licha ya kuwa na ongezeko la idadi ya vifo, WHO imesema idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani imepungua kwa miaka ya hivi karibuni.

WHO imetoa ripoti hii ili nchi kuweka jitihada za usalama wa barabarani.

Hii ikiwa ni pamoja na uwepo wa sheria sahihi za kupunguza mwendo, ufungaji mikanda na viwango vya magari.

Ulaya na Marekani zimeshuhudia kuona ajali za barabarani zikipungua.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii