Mohammed Abdullahi Farmajo: Wabunge wa Somalia waandaa hoja ya kutokuwa na imani na Rais

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Farmajo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Farmajo

Wabunge nchini Somalia wamewasilisha hoja bungeni ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Mohammed Abdullahi Farmajo.

Mmoja wa wabunge ambaye amechochea hoja hiyo Abdifitah Ismail Dahir ameiambia BBC wanamtuhumu Rais kwa uhaini baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa na kiuchumi na Ethiopia na Eritrea.

Amesema Rais ameshindwa kuwashirikisha taarifa wenzie kuhusiana na makubaliano yanayohusisha bandari za Somalia.

Wanamlaumu pia Rais kwa madai ya kuwarejesha wahalifu isivyo halali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamesababisha uharibifu Somalia

Wabunge wapatao 92 wanapaswa kusaini hoja hiyo ya kutokuwa na imani na Rais, kuweza kuwasilisha kwa Spika, ili aruhusu kuanza kwa mjadala.

Mizozo ya kisiasa ni jambo la kawaida nchini Somalia na utata huo wa hivi karibuni umekuja wakati serikali ikikosolewa kwa kuingilia kati uchaguzi wa majimbo.

Mohamed Farmajo ashinda urais Somalia

Farmajo asema atalipiza kisasi kwa kundi la al-shabab

Marais wa zamani waungana na Farmajo Somalia

Licha ya kuchaguliwa kwa Rais Farmajo kuingia madarakani mwaka uliopita na baadhi ya watu kupata matumaini, lakini bado hali ya kisiasa nchini Somalia inaonekana haijatulia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii