Jarida la Time limemtunuku Jamal Khashoggi na waandishi wengine duniani kuwa watu wenye ushawishi kwa mwaka 2018

Time covers featuring Jamal Khashoggi and staff from the Capital Gazette Haki miliki ya picha Time

Waandishi waliouwa na kufungwa jela, wametajwa kuwa kama watu wlio na ushawishi mkubwa zaidi kwa mwaka 2018 na jarida maarufu la Time.

Jarida hilo limetoa ukurasa wa mbele wa aina nne tofauti kwa heshima ya waandishi waliokumbana na madhila mbalimbali mwaka huu kutokana na kazi zao.

Kati ya hao yupo Jamal Khashoggi aliyeuawa Oktoba 2 ndani ya ubalozi wa Saudia Arabia jijini Istanbul, Uturuki.

Wengine niwaandishi wa Capital Gazette, jarida la nchini Marekani ambapo waandishi watano waliuawa, pamoja na Maria Ressa kutoka Ufilipino na Wa Lone na Kyaw Soe Oo kutoka nchi ya Myanmar.

Jarida la Time limesema limewachagua hao "kutokana na kuingia kenye dimbwi kubwa la hatari kwa kuusaka ukweli mkubwa, kwa kunyanyua sauti zao".

Jamal Khashoggi

Jamal Khashoggi alikuwa mwandishi maarufu na kinara wa kuikosoa serikali ya kifalme ya Saudia.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2.

Watu wengi katika jamii ya kimataifa wanaamini Mauaji hayo yaliamuriwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Khashoggi alikimbilia nchini Marekani akihofia maisha yake mwaka jana. Akiwa Marekani alikuwa akiandika makala kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo aliendeleza harakati zake za kumkosoa Mohammed bin Salman. Alienda Istanbul kushughulikia mchakato wa ndoa na mchumba wake wa Kituruki.

Rais wa Marekani Donald Trump amejaribu kuukingia kifua utawala wa Saudia na bin Salman. Shirika la ujasusi la CIA linadaiwa kuhitimisha kuwa bin Salman alihusika kwenye mauaji, japo Trump alidai kuwa CIA hawakutoa hitimisho hilo. Lakini maseneta wa Marekani wanaamini kuwa mwanamfalme huyo alihusika.

Capital Gazette

Mtu mwenye silaha aliingia kwenye ofisi ya gaazeti hilo jimboni Maryland, Julai 28 na kuua wafanyakazi watano wa gazeti hilo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa na hasira na gazeti hilo kutokana na kushindwa kwa shauri alilolistaki gaazeti hilo kwa kumkashifu mwaka 2012.

Pamoja na tukio hilo la kutisha na kupoteza wafanyakazi wenzao, waandishi walionusurika walitumia maegesho ya magari kuandaa toleo la siku iliyofuata la gazeti hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandishi wa Capital Gazette wakiwa wanaandaa toleo la gazeti lao kwenye maegesho ya magari siku moja baada ya wenzao watano kuuawa.

Washindi wengine

Bi Ressa ni mhariri wa Rappler, ambao ni mtandao wa habari nchini Ufilipino. Mtandao huo upo mstari wa mbele kumkosoa raisi mbabe wa nchi hiyo Rodrigo Duterte. Waandishi wa shirika la habari la Reuters Wa Lone na Kyaw Soe Oo walifungwa kwa kuandika habari za uchunguzi dhidi ya mauaji ya waislamu ya Rohingya.

Haki miliki ya picha Time

Jarida hilo lilianzisha utaratibu wa kumtunuku mtu mwenye ushawishi kwa mwaka kuanzia 1927. Kwa miaka mingi washindi huwa watu ambao wameshawishi matukio ya mwaka husika iwe kwa wema au ubaya.

Mara chache washindi huwa kundi, kama ilivyokuwa 2011 kwa waandamanaji katika nchi za Arabuni kwenye vuguvugu la mapinduzi ya raia dhidi ya serikali za kiimla na mwaka 2014 kwa watu waliopambana dhidi ya ugonjwa wa Ebola. The magazine's tradition - begun in 1927 as "Man of the Year" - recognises the person who "for better or for worse... has done the most to influence the events of the year".

The great majority of people selected have been individuals - but by no means all. In 2014, "Ebola fighters" were recognised while in 2011 "The Protester" acknowledged the significance of the so-called Arab Spring.

Mshindi wa 2006 alikuwa ni "Wewe", pamoja na kava la mbele la kioo, ili kutoa taswira ya umuhimu na nguvu ya maudhui ya mtandao yatokanao kwa watu wa kawaida. with a mirror cover design, reflecting the importance of user-generated internet content.

Mada zinazohusiana