Manchester United itamenyana na Liverpool siku ya Jumapili.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
Image caption Meneja wa Manchester United Jose Mourinho

Meneja wa timu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa kikosi cha timu yake bado hakijafikia hadhi ambayo anahitaji iwe, wakati huu wanapojiandaa kumenyana na Liverpool katika uga wa Anfield siku ya Jumapili.

Man U iko alama 16 nyuma ya vinara Liverpool, baada ya kushinda mechi moja tu ya awali kati ya tano ya ligi kuu ya League.

Mourinho, ambaye alichukua uongozi wa Timu hiyo mwezi Mei 2016, alisema: "Tuna wasiwasi!''

"Tunakwenda na wachezaji ambao tunao na kikosi ambacho kiko tayari na uwezo wa kwenda vitani."

Mourinho alishinda kombe la EFL na lile la Ligi kuu ya Uropa, katika mkondo wa kwanza huko Old Trafford.

Tangu wakati huo, mtindo wa usakataji kabumbu wa timu hiyo uliingia doa, na kumekuwa na ukosoaji mkubwa kuhusu rekodi ya Paul Pogba, ambaye kusajiliwa kwake, kulikuwa cha kiwango cha Pauni Milioni 89 na Romelu Lukaku, ambaye kima chake kiligharibu Pauni Milioni 75.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Paul Pogba, alisajiliwa kwa kima cha pauni Milioni 89

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesifiwa kwa namna ambavyo timu yake inavyosakata dimba, lakini bado hawajashinda chini ya mkufunzi huyo wa Ujerumani ambaye alianza kuongoza timu hiyo Mwezi Oktoba 2015.

Hata hivyo, aliongoza kikosi chake kushinda kombe la ligi kuu mwaka 2016 na fainali ya ligi kuu ya mchuano wa bara Uropa, pale Liverpool ilipopoteza mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid.

Alipoulizwa ikiwa kiasi cha pesa ambacho wapinzani wao north-west walitumia msimu uliopita, ulikuwa tofauti kati ya timu hizo mbili, Bwana Mourinho alijibu: "sio tu matumizi ya pesa na kuimarisha kikosi cha soka''.

"Ni sawa na nyumba. Sio kununua fanicha, ni lazima ufanye kazi, unatumia pesa katika kununua fanicha ya hali ya juu."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii