Msako mkali dhidi ya makanisa ya kikristo umeanza China na kuzua taharuki

Wang Yi akihubiri ndani ya kanisa la Early Rain Covenant Haki miliki ya picha Facebook/Early Rain
Image caption Wang Yi ni kiongozi maarufu wa kanisa moja lisilo rasmi nchini China

Hatua ya hivi karibuni ya msako mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China umesababisha taharuki kubwa kwamba serikali ya nchi hiyo inaonesha ubabe wake wa kuwakandamiza Wakristo.

Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi mmoja maarufu pamoja na mkewe. Wote ni wamiliki wa kanisa la Early Rain Covenant lililoko katika jimbo la Sichuan. Wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la kuhujumu utendakazi wa serikali ya kikomunisti ya China na kwenda kinyume na maadili ya Wachina.

Juamamosi asubuhi, kikosi cha polisi kilivamia darasa moja la kidini lililokuwa likiwapa mafunzo watoto ndani ya kanisa la Rongguili huko Guangzhou.

China ni nchi isiyomuamini Mungu, japo mamlaka zinazesa zinatoa uhuru wa kuabudu.

Lakini kwa miaka mingi utawala wa nchi hiyo umechukua hatua dhidi ya viongozi wa kidini, ambao wanaonekana kutishia mamlaka au kuyumbisha uongozi wa taifa, ambayo kwa mjibu wa shirika la Human Rights Watch, ""Hufanya kejeli kwa madai ya serikali kwamba inaheshimu imani za kidini".

Serikali inawashinikiza wakristo kujiunga na mojawepo ya makanisa makubwa matatu inayoonyesha uzalendo kwani zimepigwa msasa na serikali pamoja na chama tawala cha Kikomunisti, huku yakiongozwa na makasisi walioidhinishwa na serikali.

Kuwanyamazisha wakosoaji

Licha ya haya, idadi ya wakristo inaoongezeka kila uchao hasa katika miaka ya hivi karibuni. Kufikia sasa inakadiriwa kuwa China inao zaidi ya wakristo milioni 100, wengi wao wakiabudu ndani ya makanisa yaliyoko katika vyumba vya chini kwa chini.

Wang Yini mmojawepo wa viongozi wa makanisa kama hayo- Early Rain Covenant , lililoko Chengdu, makao makuu ya mkoa wa south-western Sichuan.

Haki miliki ya picha Facebook/Early Rain
Image caption Kanisa la Early Rain Covenant, limeweka picha hii ya maombi yao katika mtandao wa kijamii wa Facebook

Kanisa hili ni la ajabu kwani wao hufanya ibada yao hadharani na kisha kujipiga picha na kuweka kwenye mitandao yao ya kijamii, pamoja na mafunzo yao. Kanisa hilo linasema kwamba, lina jumla ya wafuasi 800 kote mjini humo. Pia inamiliki shule kadha.

Mchungaji Wang pia ni miongoni mwa wasemaji wakuu sana nchini China- amekuwa akikosoa zaidi hatua ya serikali ya china ya kudhibiti dini, na imekuwa ikiandaa ombi la kupinga sheria mpya iliyoanzishwa mwaka huu ambayo inaruhusu masharti magumu ya kuchunguza makanisa yote na kuzipiga marufuku makanisa ambayo yatakiuka sheria hiyo.

Mnamo Disemba 9, 2018, polisi walivamia kanisa na kisha kumtia mbaroni Mchungaji Wang na mkewe Jiang Rong. Siku mbili zilizofuatia, zaidi ya wafuasi wake 100, akiwemo msaidizi wa Wang, walikamatwa, na kisha kuchukuliwa.

Mmojawepo wa kanisa hilo, ambaye ameomba kutotambuliwa kwa hofu ya kukamatwa, ameiambia BBC kuwa, mlango wa kanisa hilo umevunjwa, maskani ya waumini wa kanisa hilo kupekuliwa, na baadhi ya wengine "wanazuiliwa majumbani mwao au kufuatwa kila waendako na walinda usalama".

Haki miliki ya picha Facebook/Early Rain
Image caption Kanisa hilo limeweka mitandaoni picha zinazoonyesha mateso waliyopitia wakiwa katika korokoro za polisi

Muumini huyo wa kike anasema polisi na maafisa wengine wakuu serikalini, wamekuwa wakifika majumbani mwao, kuwashinikiza kutia sahihi stakabadhi za kuwataka kuondoka kwenye kanisa hilo na pia kuwaondoa wanafunzi wao kutoka kwenye shule inayomilikiwa na kanisa hilo.

"Siku ya Jumapili, baadhi ya waumini walijaribu kukusanyika maeneo mengine kwa ajili ya ibada, lakini wakakamatwa. Jumba la kanisa limezingirwa na polisi walio na sare rasmi na baadhi wakiwa na mavazi ya kiraia, huku wakimzuia mtu yeyote kufikia majengo hayo au hata kuendesha ibada."

Knaisa linadai kuwa, baadhi ya waumini wake waliokamatwa na kisha baadaye kuachiwa huru, waliteswa vibaya.

China kupiga marufuku harusi za kifahari

Saa 48 tangu alipokamatwa, kanisa lake lilichapisha barua iliyoandikwa mapema, kutoka kwa mchungaji huyo, ya kutaka aachiwe huru ikiwa jambo kama hilo linaweza kumpata.

Ndani ya barua hiyo, anasema kwamba, anaheshimu utawala wa China na hana kwa njia yoyote "nia ya kubadilisha mkondo wowote wa kisiasa au sheria za taasisi ya China".

Lakini akaongeza kusema kuwa, "amejawa na hasira na kutoridhishwa na namna utawala wa kikomunisti unavyowatesha na kuwahujumu wafuasi wa kanisa lake".

"Kama mchungaji wa kanisa la Kikristo, napinga kabisa tena hadharani dhulma hizi za kinyama na mateso dhidi ya waumini. Wito wangu nilioupokea ni kutumia njia zozote zisizotumia uhasama, kupinga kabisa sheria za kibinadamu ambazo zinakataa kuheshimu sheria za Biblia na Mungu," amesema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jin Mingri amepinga shinikizo la serikali la kuweka kamera maalum ya CCTV kwenye kanisa lake la Zion mjini Beijing

Kote maeneo ya Guangzhou, milango yote ya kanisa la Rongguili imefungwa, na jamii kuzuiliwa kwenda makanisani.

Siku ya Jumamosi iliyopita, darasa la watoto wanaojifunza biblia lilifungwa na polisi.

Walioshuhudia wanasema kwamba, walisema kanisa hilo na mkusanyiko huo ni haramu, walichukua biblia na vifaa vingine vya kanisa na kisha mlango ukafungwa.

Maafisa wa ulinzi walichukua majina ya wote waliokuwepo, vifaa vya mitambo ya kanisa huku wote waliokuwepo wakitakiwa kupeana simu zao.

Msako wa urembo bandia China

Mwezi Septemba, kanisa la Zion, mojawepo ya kanisa kubwa mno mjini Beijing ulifungwa.

"Nina hofu kuwa hili halitamalizika hivi karibuni na utawala hauko tayari kutanzua matatizo hayo."

Pia kumekuwa na misururu ya kubomoa majengo ya kanisa, kuondoa misalaba au matendo ya kamatakamata ikifanyika kote mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch, linasema kuwa mateso dhini ya waumini wa makanisa ya Early Rain na Rongguili, yanaonyesha wazi kuwa, Cchini ya utawala wa Rais Xi Jinping, China inaendeleza ukandamizaji na udhibiti wa kila namna dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption China inataka wakristo kuabudu kwenye makanisa yanayoungwa mkono na serikali, ili kuchunguzwa kwa karibu

"Huku mataifa mengi duniani yakijiandaa kwa siku kuu ya Krismasi na Mwaka mpya, tunaziomba mataifa ya dunia kuendelea kuchunguza kwa undani kabisa hali ya uhuru ibada nchini China, na kulaani dhidi ya uovu wanaotendewa wakristo na utawala wa China," Mtafiti mmoja mkuu wa Hong Kong, Yaqiu Wang amesema.

Mfuasi mmoja wa kanisa la Early Rain, ambaye hakutaka kutajwa, amesema kwamba swala la Three-Self Patriotic churches ni la "kutamausha", akisema "hazitangazi ujumbe wa ukweli, lakini wanasambaza maoni ya kukipenda chama tawala, na kupenda nchi".

Haki miliki ya picha Early Rain
Image caption Huku makanisa yao yakiwa yamefungwa, wafuasi wa dhehebu la Early Rain,, jumapili iliyopita, wanaendesha ibada yao nje

Mkristo mmoja huko Chengdu ameiambia BBC kuwa, makanisa kama hayo "yanampinga Yesu Kristo, na injili yake".