Uchaguzi DRC: Kwa nini wapiga kura hawaamini mfumo wa elektroniki

Moto ulizuka kati ya moja ya maghala ya tume ya uchaguzi mjini Kinshasa. Haki miliki ya picha Getty/JOHN WESSELS
Image caption Moto ulizuka kati ya moja ya maghala ya tume ya uchaguzi mjini Kinshasa.

Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inaelekea kupiga kura tarehe 23 Desemba kumchagua rais mpya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001.

Rais wa sasa Joseph Kabila anaondoka madarakani na wakati siku ya kupiga kura inakabiria, kuna wasi wasi kuhusu vile kura zitapiwa kwenye nchi hiyo kubwa - karibu ukubwa wa Magharibi mwa Ulaya.

Mapema Alhamisi siku kumi tu kabla ya uchaguzi, moto uliteketeza moja ya maghala makuu ya kuhifadhi vifaa vya kupigia kura, na kuharibu zaidi ya thuluthi mbili ya vifaa vya kupigia kura kwenye mji mkuu Kinshasa.

Kilichosababisha moto huo hakijathibitishwa.

Haki miliki ya picha Getty/JOHN WESSELS
Image caption Vifaa vya eletroniki vitatumiwa nchini DRC

Wakati wote wa kampeni, kutumika kwa mashine za eletroniki kwa mara ya kwanza imekuwa mjadala mkubwa.

Felix Tshisekedi, mmoja wa viongozi wa upinzani anayewania urais, aliibua wasi wasi kuhusu vifaa hivyo vya kupigia kura.

Kundi lingine kuu la upinzani likiongozwa na Martin Fayulu limetishia kususia uchaguzi.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, hivi majuzi aliionya DR Congo dhidi ya matumizi ya vifaa hivyo vya elektroniki vya kupigia kura na kutumia njia iliyoaminiwa yenye uwazi na iliyofanyiwa majaribio ya kutumia makaratasi ya kupigia kura.

Haki miliki ya picha Getty/ALEXIS HUGUET
Image caption Martin Fayulu, mgombea urais wa upinzani

Wapiga kura wana wasi wasi wa nini?

Upigaji kura nchini DR Congo umekumbwa na jinamizi la usafiri na uchaguzi wa awali umekumbwa na changamoto kubwa.

Kuna wapiga kura milioni 46 waliojiandikisha kuwapigia kura wagombea 34, 900 kwa viti 500 vya kitaifa, viti 715 vya mikoa na 21 vya urais na vituo 21,100 vya kupigia kuta kote nchini.

Tume ya uchaguzi ina mpango wa kusambaza vifaa vya eletroniki 105,000 kutoka kwa kampuni ya Korea Kusini Miru Systems.

Vifaa sawa na hivyo vimetumiwa nchini Ubelgiji, Brazil, India, Namibia na Venezuela.

Lakini ndiyo mara ya kwanza mashine za aina hii zinatumiwa na kuibua wasiwasi kuwa havijafanyiwa majaribio kwa hali kama hii.

Haki miliki ya picha CENI
Image caption Picha za magari yaliyoteketea moto wakati moto ulichoma ghala la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura

Vifaa hivi vinafanya kazi kwa njia gani?

Kila mpiga kura anaingia kituo cha kupigia kura na kuwachagua wagombea kwa kutumia kifaa kinachofanana na tablet.

Chaguo na mpiga kura kisha litachapishwa kwenye karatasi, ambayo mpiga kura husalimisha. Karatasi hiyo sasa ndiyo uhesabiwa. Mashine hizo uhifadhi kumbukumbu kusaidia kuthibitisha matokeo.

Ikiwa matokeo yatatofautiana kutakuwa na pingamizi na kuchanganyikiwa - licha kuwa nyakati kama hizo ni makaratasi yataamua, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Kukosa kujaribiwa

Uchunguzi uliofanywa mara mbili imeibua wasiwasi kuhusu mfumo huo wa elektroniki ambao utatumiwa kwenye uchaguzi nchini DRC.

Uchunguzi uliofanyiwa vifaa hivyo na Westminster Foundation for Democracy unasema havijafanyiwa majaribio yanayostahili na kuwa kuna uwezekano kuwa kunaweza kutokea kuchelewa na kutumiwa kwa njia mbaya.

Mtengezaji wa mashine hizi, Miru Systems amejibu madai ya shaka za usalama. "Madai yaliyotajwa si ya ukweli," aliandika mkurugenzi Ken Cho kwa njia ya barua pepe kwa Washington Post.

Haki miliki ya picha Getty/JOHN WESSELS
Image caption Thuluthi mbili ya vifaa vya kupigia kura viliharibiwa kwenye moto

Vifaa hivi vishatumiwa wapi?

Data kutoka taasisi ya kimataifa ya Demokrasia inaonyesha kuwa nchi 33 kwa sasa zinatumia njia fulani kwa kupiga kura kwa njia ya elktroniki.

Katika baadhi ya nchi hakujakuwa na shaka.

Kwenye uchaguzi nchini Venzeula mwaka uliapita mkuu wa kampuni iliyoipa mashine hizo alisema idadi ya wapiga kura ilikuwa imeongezwa kwa karibu kura milioni moja

Pia kumekuwa na wasi wasi nchini Argetina

Mada zinazohusiana