Wakaliwood: Filamu za bei nafuu za Uganda zinavyotayarishwa

Mtengenezaji maarufu wa filamu nchini Uganda aliyehamasisha sekta nzima ya filamu inayojulikana kama Wakaliwood Nabwana Isaac Godfrey Geoffrey sasa hivi anashughulikia filamu yake yenye gharama ya juu zaidi.

Bajeti yake? Dola elfu mbili. Anatumia vifaa vinavyopatikana kwa rahisi kama vile bunduki bandia, helikopta zilizotengenezwa kutokana na vyuma chakavu, lakini wizi wa hakimiliki sasa umekuwa tishio kwa biashara yake.

Mwandishi wa BBC Charles Gitonga alijaribu kucheza moja ya filamu hizo.