Tsunami yapiga Indonesia, watu zaidi ya 160 wauawa na zaidi ya 700 kujeruhiwa

Anak Krakatau erupting, 19 July 2018 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wanasema Anak Krakatau huenda ilisababisha tsunami

Takriban watu 168 wameuawa na wengine 745 kujeruhiwa baada uya tsunami kukumba miji ya pwani nchini Indonesia kwa mujibu wa serikali.

Mawimbi ya tsusami yaliwasili usiku bila onyo lolote, na kuharibu mamia ya nyumba.

Maafisa wanasema tsunami hiyo huenda ilisababishwa na maporomoko ya ardhi chini ya bahari baada ya kulipuka kwa volkano ya Anak Krakatau.

Eneo la Sunda Strait kati ya visiwa vya Java na Sumtara huunganisha bahari ya Java na bahari ya Hindi.

Haki miliki ya picha Oystein Lund Andersen
Image caption Mitaa iliyofurika maji baada ya tsunami

Habarari za sasa zinasemaje?

Idara inayohusika na majanga imeonya watu kukaa mbali na pwani kutonana na hofu kuwa tsunami nyingine inaweza kutokea.

Tsunami ya Jumamosi ilipiga fukwe kadhaa likiwemo eneo la kustarehe la Tanjung Lusung magharibi mwa kisiwa cha Java.

Vifo vimeripotiwa maeneo ya Pandeglang na Serang huko Java, na mkoa wa Lampung huko Sumatra. Maafisa wanahofu kuwa idadi ya waliokufa huenda ikapanda.

Image caption Ramani
Haki miliki ya picha Gallo Images/Orbital Horizon/Copernicus Sentin
Image caption Picha za satellite zikionyesha mlima Anak Krakatau ukilipuka Agosti

T

Mada zinazohusiana