Kumbukumbu: Zura Karuhimbi ni mwanamke aliyeweza kuokoa mamia ya watu katika mauaji ya kimbari Rwanda

Zura Karuhimbi in 2014

Chanzo cha picha, Jean Pierre Bucyensenge

Zura Karuhimbi hakuwa na silaha yeyote ya kujilinda wakati wanaume waliokuwa na silaha walipoizunguka nyumba yake na kumtaka awakabidhi watu aliokuwa amewahifadhi nyumbani mwake.

Mwanamke huyo alikuwa anajulikana kuwa na nguvu za giza.

Hali iliyowafanya kundi hilo la wauaji kuwa na uoga na kumfanya mwanamke huyo mzee kuwaokoa watu zaidi ya 100 kuwa salama wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Watusi wengine laki 8 na wahutu waliuwawa katika mauaji ambayo yalitokea mwaka 1994 akiwemo mtoto wake wa kwanza wa kiume na binti yake.

"Wakati wa mauaji ya kimbali , niliona giza katika moyo wa mwanadamu" maelezo ya Karuhimbi .

Alizaliwa katika familia ya waganga wa jadi

Karuhimbi alikufa kwa amani siku ya jumatatu, akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Musamo kilichopo upande wa mashariki wa mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Hakuna aliyekuwa anajua bibi huyo ana umri gani?

Lakini kwa muonekana unaweza kumkadiria kuwa anazidi miaka 100.

Huku askari wa kihutu walimfahamu kama 'Interahamwe' ambaye alifika kijijini hapo akiwa msichana mdogo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Askari wa kihutu wakikimbia barabarani wakiwa na askari wa Ufaransa mwaka 1994 mwezi Juni

Kwa mujibu wa simulizi nyingi zilizoandikwa kuhusu maisha ya Karuhimbi, kuzaliwa katika familia ya waganga wa jadi mnamo mwaka 1925.

Hii inaweza kudhihirisha kuwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yalimrudisha katika hali aliyopitia akiwa mdogo.

Wakati ambapo waberigiji walipoamua kuwagawa wanyaruanda katika makundi mawili kwa kuwagawia vitambulisho vinavyobainisha mhutu au mtusi.

Familia ya Karuhimbi ilikuwa ni wahutu, kundi ambalo lilikuwa na watu wengi nchi Rwanda.

Kundi la waliokuwa wachache ambao ni watusi walijulikana kama ndio imara na kutokana na sababu hiyo , walikuwa wanapata ajira nzuri na fursa ya elimu kutoka kwa wakoloni.

Mgawanyiko huo ulileta chuki kati ya makundi hayo: Karuhimbi alikuwa bado mdogo mwaka 1959, wakati ambapo mfalme wa watusi Kigeri V, akiwa pamoja na maelfu ya watusi walipolazimika kukimbilia nchi ya jirani ya Uganda mara baada kile kilichofahamika kama mapinduzi ya wahutu nchini Rwanda.

Wakati shambulio la kwanza lilipotokea baada ya kuanguka kwa ndege ya rais mwenye asili ya kihutu Juvenal Habyarimana, mwaka 1994, huu ndio wakati ambao mama huyo alianza kuwa hatari.

Lakini hakuwa anajua ni mambo gani mabaya ambayo yangeweza kutokea, wanaume wa kihutu waliowaowa watusi waliamua kuwarudia wake zao ili kuzuia janga lingine lisitokee.

"Nilikuwa nasema kwamba kama watakufa basi na mimi pia nitakufa, Hata kama ningejua mtuhumiwa yeyote , nisingeweza kumzuia." Mwanamke huyo alisema hayo katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari.

'Walikuwa wanajichimbia makaburi yao wenyewe'

Vyumba viwili vidogo vilivyopo kijijini Musamo, kwa haraka vilikuwa sehemu salama kwa watusi, Waburundi na hata wazungu watatu walijificha humo wakati wa mauaji ya kimbari.

Makundi ya watu yaliripotiwa kuwa walikuwa wamejificha chini ya kitanda na eneo lingine la siri juu ya paa.

Huku wengine walisema kuwa alikuwa amewachimbia shimo kuwaficha.

Chanzo cha picha, Jean Pierre Bucyensenge

Maelezo ya picha,

Karuhimbi akiwa pamoja na mwanaume, aliyewahi kumuokoa katika mauaji ya kimbari

Baadhi yao walikuwa watoto ambao walichukuliwa kutoka kwa mama zao waliokufa, alisema hivyo.

Kama ilivyokuwa kwa umri wake kuwa hakuna mtu aliujua vilevile katika nyumba yake hakuna aliyefahamu ni watu wangapi walijificha humo.

Karuhimbi alimwambia mwandishi wa habari wa Rwanda Jean Pierre Bucyensenge katika kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kuwa ,

"Silaha pekee ya Zura ilikuwa ni kuwatisha wauaji kuwa atawaloga wao pamoja na familia zao, " bwana Bucyensenge alieleza.

Hassan Habiyakare alidai kuwa watu waliogopa uchawi na ndio njia pekee bibi huyo aliyoitumia na anaikumbuka vizuri ,' kuna mtu alikuwa anaogopa kuokolewa na mchawi '.

Zura aliwaambia askari wa kihutu kuwa watajaribu kufika katika himaya yake basi watapambana na neno la Mungu, Walishikwa uoga na waliamini kuwa maisha yao yaliokolewa kwa ajili ya siku nyingine.

Karuhimbi mwenyewe alileza namna ambavyo alikuwa akifanya chochote ilimradi tu apate njia ya kuwatishia wauaji hao waondoke.

Tahadhari aliyokuwa anatoa ilifanya kazi.

Wakati ambapo mauaji ya kimbali yalipomalizika mwezi Julai , watusi waliweza kuingia Kigali na kupambana na waasi.

Kila mtu ambaye alimuomba msaada Karuhimbi , ambaye alihatarisha maisha yake ili kuwaokoa waliweza kupona.

Maisha yaliendelea huku akiwa ni mwanamke ambaye anaomboleza kupotea kwa mtoto wake katika vurugu hizo na binti yake ilijulikana kuwa aliwekewa sumu akafa.

Pamoja na umaarufu mkubwa alioupata kuwa alikuwa mchawi lakini hakuwa mchawi na wala hakuwahi kuwa mchawi.

"Ninaamini kuwa kuna Mungu mmoja na njama ya kutumia nguvu za giza aliitumia ili kuokoa maisha ya watu," alimwambia Bucyensenge mwaka 2014.

"Mimi sio mganga wa kienyeji wala mchawi."

Mwaka 2006, bibi huyo alitunukiwa tuzo ya kupambana na mauaji ya kimbari . Tuzo hiyo ilimpa nafasi ya kusimulia namna alivyookoa watu wengine 50 katika miaka ya nyuma.

Nishani yake alikuwa anahifadhi chini ya mto wa kulalia

Kwa mujibu wa Karuhimbi katika mauaji ya makundi hayo mawili yaliyotokea 1959, alimshauri mama mmoja wa kitusi mwenye mtoto wa miaka miwili kutoa shanga alizokuwa amevaa shingoni na kuzifunga katika nywele za mtoto wake.

Alimwambia hivyo kwa sababu kipindi hicho walikuwa wanaua watoto wakiume hivyo , nywele za mtoto huyo zikifungwa atajulikana kuwa ni mtoto wa kike.

Chanzo cha picha, JP Bucyensenge

Maelezo ya picha,

Zura Karuhimbi aliivaa medali yake kila wakati

Na huyo mtoto alipona na baadae ndio mwanaume ambaye alimkabidhi nishani , Rais Paul Kagame.

Karuhimbi hakuwahi kujua ni nini kilitokea kwa watu wengine ambao aliwahi kuwasaidia.

Maelezo ya picha,

Paul Kagame aliwaongoza waasi wa kitusi kumaliza mauaji ya kimbari na baadae akawa rais mwaka 2000

Medali au nishani aliyopewa na Kagame mwaka 2006 ilibaki kuwa tunu kubwa kwake.

Alikuwa anaivaa kila wakati na kuiweka vizuri chini ya mto wakati anapolala.

Na wale ambao waliwahi kumuona walitamani simulizi ya mwanamke huyo wa kihutu ambaye aliacha kila kitu ili kuwaokoa wengine kuweza kuandikwa.

"Mwanamke huyu alihatarisha maisha yake ili kuokoa maisha ya wengine," Bucyensenge aliiambia BBC.

"Simulizi ya maisha yake inaonesha namna ambavyo mtu anaweza kuwa na utu hata katika kipindi kigumu."