Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 27.12.2018: Hazard, Isco, Kovacic, Costa, Aarons, Doucoure, Hernandez

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eden Hazard

Real Madrid wanataka kumpa ofa mchezaji wa Chelsea raia wa Uhispania Isco, 26, na kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic ambaye tayari yuko kwa mkopo huko Stamford Bridge - kama sehemu ya makubaliano kumsaini mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27. (Onda Cero, via Metro)

Juventus hawawezi kumuuza kiungo wa kati wa Brazil mwenye miaka 28 Douglas Costa, ambaye amehusishwa na Manchester City na Manchester United, mwezi Januari. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Isco

West Ham wametoa ofa ya pauani milioni 6.5 kwa kiungo wa kati wa Chile Gary Medel, 31, aliyekatalikwa na klabu ya Uturuki ya Besiktas. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Tottenham mbelgiji mwenye miaka 31 Mousa Dembele, ambaye mkataba wake unaisha anatafutwa na meneja wa Monaco Thierry Henry. (Le Sport 10 - in French)

Watford wana hofu wanaweza kumpoteza kiungo wa kati Mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25, kwenda Paris St-Germain mwezi ujao na wanaweza kumwendea aliyekuwa mchezaji wa Nice Mfaransa Adrien Tameze, 24, achukue nafasi yake. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Douglas Costa

Mkurugenzi mkuu wa CSKA Moscow Roman Babaev anaaminia mchezaji wa mkopo wa Everton Nikola Vlasic, 21, anataka kubaki kwenye kalabu lakinia anasema klabu haitakuw na uwezo wa kumsaini kabisa mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia. (Liverpool Echo)

Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez hafikirii kuwa klabu hiyo itakuwa tayari kumsaini mchezaji mapema mwezi Januari. (Chronicle)

Mmiliki wa Nottingham Forest Evangelos Marinakis anafikiria kumfuta meneja Aitor Karanka baada ya mechi bila ushindi ripoti za mzozo wa wachezaji kwenye klabu. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ernesto Valverde

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde bado haijakijulisha klabu hiyo ya Uhispania ikiwa ataendelea na mkataba kwa mwaka wa tatu huko Nou Camp. (Marca)

Atletico Madrid wanajaribu kuuuzuia Bayern Munich kufufua kipenge cha kukata mkataba wa mlinzi mwenye miaka 22 mfaransa Lucas Hernandez cha euro milioni 80 mwezi Januari. (Marca)

Meneja wa West Brom Darren Moore anasema hana wasi wasi kuhusu uwezekano wa kuwindwa na vilabu vya Ligi ya Premia mchezaji straika Jay Rodriguez, 29. (Times - subscription required)