Walioandikisha historia na taarifa kuu barani Afrika mwaka 2018

Screen grab of PM doing press-ups

Chanzo cha picha, Walta TV

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamrisha wanajeshi waliomtisha kufanya mazoezi

Katika mfululizo kwa barua kutoka Afrika, mwandishi wa habari raia wa Ghana Elizabeth Ohene anaangazia baadhi ya masuala makuu barani Afrika 2018.

Si kila siku unaweza kumuona Waziri Mkuu akiongoza kundi la wanajeshi wakifanya mazoezi, hasa wakati wanajeshi hao wamejaribu kuingia kwa nguvu ofisini kwake kupinga kutolipwa mishahara.

Ni aina ya hatua kama hizi ambazo ziligeuka kuwa mapinduzi.

Lakini Abiy Ahmed amekuwa akifanya mambo ambayo yalionekana kuwa magumu tangu aliingia madarakani kama waziri mkuu wa Ethiopia mwezi Aprili.

Ana miaka 42 na kiongozi mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika.

Ethiopia ilionekana kama taifa la kiimla lililopuuza ukosoaji na kudumisha uhasama na jirani wake Eritrea.

Lakini miezi michahe baada ya kuingia ofisini Bw Abiy alindoa amri ya hatari, akawafungulia melfu ya wafungwa wa kisiasa, akawaruhusu watoro kurudi nyumbani na kufungua mamia ya mitandao na Televisheni.

Amani na hasimu wa miaka mingi

Waziri mkuu alimaliza hali ya vita na Eritrea kwa kukubali kusalimisha ardhi ya mpakani na kuboresha uhasiano na hasimu huyo wa zamani.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Sahle-Work Zewde na rais wa kwanza mwanamke nchini Ethiopia

Hii ilitokea wakati wa ziara ambayo haikutarajiwa kwenye mji mkuu wa Eritrea Asmara na akashikana mikono hadharani na rais wa Eritrea Isaias Afwerki kutangaza kumalizika vita vya miongo miwili.

Wanawake madarakani

Safari za ndege na mawasiliano ya simu yamerejeshwa na nchi hizo mbili zikaanza kupendana hatua iliyoshangaza dunia.

Na kama yoyote alikuwa anafikia mamabo ya kushangaza yalikuwa yamefikia mwisho, mwezi Oktoba Bw Abiy aliteua nusu ya wanawake kwenye baraza lake la mawazri.

Pia Ethiopia sasa na rais wa kwanza mwanamke (Sahle-Work Zewde), mwanmke jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi (Meaza Ashenafi), mwanamke mkuu wa tume ya uchaguzi (Birtukan Mideksa) na msemaji wa serikali ni mwanamke (Billene Aster Seyoum).

Afrika Kusini ni nchi nyingine ilishuhudia mabadiliko makubwa hasa tangu rais mpya Cyril Ramaphosa ashike hatamu za uongozi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Cyril Ramaphosa

Aliingia madarakani baada ya rais aliyekuwa amekumbwa na sakata kulazimishwa kujiuzulu mwezi Februari.

Wakati alianzisha hashitegi, "kitambi lazima kianguke", raia wengine wa Afrika Kusini walihisi muda wa kutabasamu umereja nchini humo

Lakinia bado kivuli cha Zuma bado kipo wakati Bw Ramaphosa anajaribu kukabliana na sakata za ufisadi zilizoibuka wakati wa mtangulizi wake .

Bw Zuma anasisitiza kuwa hana hatia na ameomba mahakana kutupa nje kesi zake 16 zilizoletwa zinazohusu ununuzi wa silaha.

Weah amatuza Wenger

Bobi Wine, mwanamuziki nyota kutoka Uganga na mbuge aliitikkiza Uganda kwa wiki chake mwezi Agosti na kuvutia dunia wakati alikamatwa na polisi akishtakiwa kwa mkosa ya uhaini.

Baada ya kuondoka nchini humo kupata matibabu kwa majeraha ambayo anadai alipata wakati alikamatwa, sasa amerudi Uganda na tamasha lake la kwanza mwezi Novemba lilikuwa ishara tosha ya umaaarufu wake mkubwa.

Mtu mzuri alitambuliwa kwa matendo yake mema wakati Denis Mukwege daktari raia wa Congo alipewa tuzo ya amani ya Nobel na mwaharakati wa Yazidi Nadia Murad.

Dr Mukwege ametajwa kuwa mtaalamu mkubwa dunai wa kutibu majeraha ya ubakaji na anafahamika kama "Doctor Miracle" kwa kazi yake nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Arsene Wenger alipata makaribisho makubwa nchini Liberia

George Weah alichaguliwa rais wa Liberia mwezi Januaria na kuonyesha heri njema kwa wale waliomsaidia katika taaluma yake ya kandanda wakati alimpa kocha wake wa zamani Arsene Wenger tuzo la juu zaidi la nchi nhiyo.

Ikiwa Nelson Mandela angekuwa hai angekuwa amefikisha umri wa miaka 100 mwaka huu na kwa kuikumbuka siku yake ya kuzaliwa mambo kadhaa yalipangwa na kufanyika kote duniani.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alielekea nchini Afrika Kusini kutoa hotuba na kulikuwa ana tamasha za kumsherehekea Madiba kama shujaawa kupinga ubaguzi wa rangi.

Hugh Masekela mpiga tarumbeta maarufu nchini Afrika Kusini alifariki mwaka huu na kuombolezwa sana.

Winnie madikizela Mandela , mke wa zamania wa Nelson Mandela aliyependwa sana na wakati mwingine mpinzani wa ubaguzi wa rangi pia naye alikufa na kufanyiwa mazisho makubwa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipewa maziko makubwa Ghana

Kofi Annan katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, alisherehekea miaka 80 ya kuzaliwa na kuendelea na shughuli zake za amani wakati aliongoza ujumbe kwenda nchini Zimbabwe kabla ya uchaguzi wa mwezi Julai. Alifariki ghafla huko Bern Uswizi mwezi Agosti.

Mwili wake ulisafiriswa kwenda nyumbani nchini Ghana ambapo alipewa maziko ya kitaifa.

Mapenzi kati ya China na Afrika yaliendelea kwenye mkutano mjini Beijing mwaka huu, Rais Xi Jinping alitanga mkopo wa dola bilioni 60 kwa nchi za Afrika.

Wamarekani walitangazawazi kuwa mipango ya China kwa nchi za Afrika sio mizuri.