Unawezaje kujizuia kunywa pombe msimu wa Siku Kuu?

pombe

Chanzo cha picha, Getty Images

Kama haunywi pombe kwasababu za kiafya au unapambana na uraibu hebu fikiria inakuwaje pale unapo lazimishwa kunywa ama kubembelezwa unywe na marafiki au ndugu.

Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa jina lengine kinafahamika kama msimu wa Siku Kuu kutokana na kufuatana kwa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka Mpya na asilimia kubwa ya wafanyakazi hupendelea kwenda likizo.

Kukutana marafiki ndugu ama familia huu ndio wakati wake. Pombe ni moja kati ya vinywaji ambavyo hutumika zaidi katika mikutano hiyo.

Hata hivyo wapo ambao ni wanyaji sana, wasio kunywa kabisa, wanao jitahidi kuacha pombe, wasio kunywa kwasababu za kiafya huenda wanameza dawa na wapo ambao wanapambana na uraibu yaani adiction hivyo hawatakiwi kuonja pombe.

Watu wote hao wanahitaji kujumuika pamoja, lakini changamoto ni pale baadhi ya wanao kunywa pombe wanaona hapana kukaa na mtu asiyekunywa pombe ni kero hivyo lazima wote wanywe.

BBC imezungumza na kijana Isack Mugisha anasema haoni sababu ya kukaa kilabuni na mtu asiye kunywa.

"Unajua unapokuta watu wanakunywa alafu ukaungana nao unaagiza soda aisee inakata stimu bora ukae nyumbani kama unajua haunywi. Raha ya bia wote tunywe afu tuyajenge taratibu hapo aah shwari," anasema Mugisha

Hata hivyo BBC imezungumza na Lomwe yeye anasema huwa anakunywa pombe kakini kwasasa hawezi kunywa pombe sababu anatumia dawa.

"Kwasasa sinywi aisee nimeugua wakati mbaya daah hapa nina dozi ya wiki mbili siwezi kabisa kunywa, washkaji wananiita ila naona bora nisiende maana hata mimi sipendi kukaa na mtu asipokuwa anatupia moto moto. Leo natoka ila wakinilazimisha kunywa pombe sijui itakuwaje ila sita kunywa," anasema Lomwe

Jinsi ya kujizuia kunywa pombe

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwingereza Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilicho uzika sana cha Reasons to stay alive anasema yeye akinywa humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.

"hata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasio kula nyama afu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo," anasema Haig

Anasema ni bora kuto kutoka kwasababu kule utashawishika tu na njianyingine ni kama vile:

  • Nenda kwenye migahawa na sio Bar
  • Fanya mazoezi tumia ule muda unaokuwa wazi
  • Weka wazi kwamba hutumii pombe
  • Epuka makundi au marafiki wanywaji
  • Tafuta starehe katika kinywaji mbadala
  • Badili sehemu ulizokuwa unaenda kupumzika awali na wajulishe watu wako wa karibu

Upweke wa kijamii

Mbali na ukweli kwamba pombe ni sehemu kubwa ama kinywaji kinacho furahiwa katika jamii zetu, utamaduni unabadilika.

Takwimu za hivi karibuni kupitia utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha London unaonyesha theluthi ya vijana wadogo hawanyi pombe kabisa.

Japokuwa vijana wadogo ambao wanasumbuliwa na afya ya akili pia wanatatizo la unywaji pombe kupita kiasi.

Jennifer Griffin, mtaalamu wa afya ya jamii lakini pia meneja wa taasisi ya huduma ya akili Turn2me anasea watu wanatakiwa kujikita katika kufanya mazoezi kama njia mbadala, lakini pia kuyapa kipaumbele mahitaji binafsi ya msingi.

"Pombe inahusishwa na wasiwasi lakini pia hali ya kukosa raha funaha na kuwa na woga. Lakini kujichanganya ndio namna vijana wadogo hufanya ili kujiunganisha na watu na kutengeneza marafiki. Wasipo jichanganya kwa kuhofia kunywa pombe wanaweza wakaanza kujitenga kisha wakaanza kuteseka na upweke".

Uelewa juu ya athari za kiafya unazidi kukua. Kila mmoja akubali. Mtu anaposema hataki kunywa pombe usimlazimishe wala usimwuulize mara mbili.