Rais Joseph Kabila: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Rais Joseph Kabila: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Rais Joseph Kabila ambaye anamaliza muda wake wa uongozi nchini DRC amezungumza na idhaa ya Kiswahili ya BBC na kuhakikishia raia wake kuwa licha ya changamoto uchaguzi unaotarajiwa kufanyika jumapili utafanyika kwa uhuru na amani.

Uchaguzi huo, unaofuatiliwa kwa karibu na Jumuiya ya Kimataifa, ulikuwa ufanyike miaka miwili iliyopita na Kabila ambaye amedumu madarakani kwa miaka 17 amekuwa akishutumiwa ndani na nje ya Congo kwa kutafuta sababu za kusalia madarakani.