Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 28.12.2018: Ramsey, Hazard, Nasri, Higuain, Pogba

Aaron Ramsey

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aaron Ramsey

Paris St-Germain wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, kuhusu kuhama mwezi Januari. Mchezaji huyo kutoka Wales hana mkataba mwisho wa msimu. (L'Equipe - in French)

Na klabu hiyo ya Ufaransa anaweka tayari pauni milioni 9 kwa ofa ya Ramsy kuwazuia Bayern Munich na Juventus. (Mirror)

PSG pia wanamfuatilia mchezaji mwenye miaka 29 kiungo wa kati wa Everton na Senegal Idrissa Gueye. (L'Equipe - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hazard

Manchester United watamfikiria meneja wa Juventus Massimiliano Allegri wanapomsaka meneja mpya wa kudumu. (ESPN)

Tottenham wanaamini Real Madrid ni tisho kubwa kuliko United kumchukua meneja Mauricio Pochettino. (Telegraph)

Lakini United hawatamtangza meneja wo mpya kabla ya mwisho wa msimu. (Talksport)

Eden Hazard bado hayuko tayari kuzungumzia mkataba mapya huko Chelsea hadi msimu ujao licha ya Real Madrid kuonyesha dalili za kumwinda mchezaji huyto wa miak 27. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Samir Nasri

West Ham wamempa Samir Nasri, 31, ofa ya mshahara wa paunia 80,000 kwa wiki hadi mwisho wa msimu huku marufuku yake ya kutumia dawa iiliyopigwa marufuku ikitarajiwa kuisha Desemba 31. (Mirror)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amesema mafanikio ya timu yake msimu huu yanamaanisha hawatamsaini mechezaji yeyote msimu ujao. (ESPN)

Beki wa Liverpool Alberto Moreno anasema hana furaha jinsi ametendewa na meneja Jurgen Klopp na anataka kurudi Uhispania wakati mkataba wake unatarajiwa kumamilika mwezi Juni. (Onda Cero, via AS)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alberto Moreno

Meneja wa Everton Marco Silva anasisitiza kuwa mshambuliaji mturuki Cenk Tosun, 27, bado ana matumaini katika klabu nhiyo. (Guardian)

Real Madrid wanataka kumsaini beki wa Real Betis Junior Firpo, 22, kama mrithi wa Marcelo lakini anakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Manchester City. (AS)

Kipengee cha mkataba wa mchezaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain kinamaanisha kwa Arsenal ilihitajika kulipa klabu ya zamani ya Southampton pauni 10,000 kwa kiungo huyo wa kati wa England kwa kila zaidi ya dakika 20 alizocheza (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paul Pogba

Beki wa Colombia Jeison Murillo, 26, anataka kuhamia kabisa Barcelona baada ya kujiunga kwa mkopo kutoka Valencia hadi mwisho wa msimu na anaweza kusainiwa kwa pauni milioni 22.6. (Marca)

Thorgan Hazard ndugu mdogo wa Eden hataruhusiwa kuondoka Borussia Monchengladbach mwezi Januari licha kuwa vilabu kadhaa vimeonyesha ni ikiwemo Tottenham, huku Chelsea ikiwa na kipengee cha kununua tena msimu huu. Bild - in German)