Colombia yachunguza njama ya kutaka 'kumuua rais wake' Iván Duque

Colombian President Iván Duque giving a speech

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha,

Rais wa Colombia Iván Duque amekuwa akiikosoa vikali serikali ya Colombia

Colombia imelalamikia kile inachodai ni njama kwa kumuua rais wake, na kusema kuwa raia watatu wa Venezuela wamekamatwa kwa kuhusika na njama hiyo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Carlos Holmes Trujillo alisema kulikuwa na njama ya kumlenga rais Iván Duque.

Bila ya kueleza zaidi, Mr Trujillo pia alisema kuwa raia watatu wa Venezuela wamekamatwa wakiwa na silaha.

Misukosuko imeongezeka kati ya Colombia na Venezuela miezi ya hivi karibuni huku maafisa wakifukuzwa kutoka nchi zote.

Mamilioni wameikimbia Venezuela kutokana na hali mbaya ya uchumi miaka ya hivi karibuni na wengi waliohama wamevuka na kuingia Colombia.

Bw Duque alichaguliwa mwezi Agosti akiahidi kuitenga nchi hiyo kidiplomasia.

Uchunguzi kuhusu uwezekano wa shambulizi hilo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bw Maduro ameilaumu Colombia kwa kupanga kumuua

Taarifa za polisi na za jeshi nchini Colombia zililiambia shirika la Reuters kuwa raia watatu wa Venezuela walikamatwa mapema Desemba wawili ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Rais Duque ametoa wito kwa nchi kumtomtambua rais wa Venezuela Nicolás Maduro baada ua uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi Mei na kumtaja kiongozi huyo kuwa dikteta.

Lakini Maduro alikuwa amedai kuwa Colombia na Marekani walikuwa wamepanga njama ya kutaka kumuua.

Rais huyo wa Venezuela alidai mwenyewe hivi majuzi kuwa mshauri wa usalama wa kimataifa nchini Marekani John Bolton mwenyewe alikuwa alihusika katika njama ya kumuua.

Kuwasili kwa ndege za Urusi za kubeba mabomu ya nyuklia nchini Venezuela kuliongeza misukosuko zaidi.