Saba Gul : Binti asiye na mikono aliyejifunza kuitumia miguu yake

Saba Gul : Binti asiye na mikono aliyejifunza kuitumia miguu yake

Saba Gul alipoteza mikono yake yote miwili katika ajali nyumbani kwao akiwa na miaka mitano.

Alidhalilishwa sana na hata baadhi wakasema hakukuwa na haja yoyote kumpeleka shuleni.

Lakini hakufa moyo na sasa akiwa na miaka 15 amekuwa akiitumia miguu yake kufanya kazi nyingi ambazo hufanywa kwa kutumia mikono, kwa mfano kula, kuandika, kupiga simu na hata kufua nguo.

Na ana ndoto kuu maishani, kutetea haki za binadamu na haki za wanawake na kubadilisha jamii Pakistan.