Utafiti: Madaktari wabaini watoto wanaotumia simu sana wanaathirika ubongo

Utafiti: Madaktari wabaini watoto wanaotumia simu sana wanaathirika ubongo

Watafiti wamegundua kwamba kuna tofauti katika ukubwa wa ubongo kati ya watoto wanaotumia sana vifaa vya kielektroniki kama vile simu, tablet na kucheza michezo ya kompyuta na wale wasiofanya hivyo.

Utafiti huo umefanyiwa Marekani ambapo imebainika kwamba sehemu ya ubongo inayoathirika ni kwenye tabaka la nje ya ubongo, kwa Kiingereza cortex.

Sehemu hiyo huhusika katika fahamu.

Utafiti huo ulibaini pia kwamba watoto wanaotumia vifaa hivyo vya kieletroniki saa mbili na zaidi wanapata matokeo duni katika masomo ya lugha na mitihani inayohitaji mtu kuwaza na kufikiria kwa undani pamoja na kuandaa na kupambanua hoja.

Mradi huo wa utafiti wa $300m uliowashirikisha watoto 4,500 unaendeshwa na Taasisi ya Taifa ya Afya Marekani.

Lengo jingine la utafiti huo ni kubaini iwapo kutazama skrini za simu na kompyuta sana unaweza kuwa uraibu.

Unaweza kusoma pia: