Kwa Picha: Miji ilivyoukaribisha Mwaka Mpya wa 2019

Shangwe, vifijo, nderemo zilisheheni miji mbalimbali watu wakisherehekea kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2019 katika majiji mbalimbali duniani, fataki nazo zikatanda angani.

Fataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London Haki miliki ya picha EPA
Image caption Fataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London
"Yellow Vest", waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris Haki miliki ya picha EPA
Image caption "Yellow Vest", waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris
Hapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin
Wanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow
Jijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya
Na hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya
Maelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Maelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung
Hapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini
Katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia
Ufilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya 'kumsaidia kuuona vyema' Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ufilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya 'kumsaidia kuuona vyema' Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon
Waumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini
Hapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan
Anga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China Haki miliki ya picha EPA
Image caption Anga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China
Sherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China Haki miliki ya picha Lintao Zhang/Getty Images
Image caption Sherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China
Na Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Na Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi
Huko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Huko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12

Unaweza kusoma pia:

Njia bora ya kutimiza malengo yako ya Mwaka Mpya

Upinzani waazimia 'kudai demokrasia' Tanzania 2019

Apandikizwa uso mpya baada ya kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi

Picha zote zina hakimiliki.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii