Kang Daniel: Mtu aliyepata wafuasi wengi wa Instagram kwa haraka zaidi

Kang Daniel and Pope Francis Haki miliki ya picha Getty Images

Kitu gani ambacho K-pop star Kang Daniel anacho kinachofanana na Papa pamoja na David Beckham?

Papa Francis na David Beckham ni watu ambao walipata marafiki milioni kwa haraka katika mtandao wa Instagram , na wiki hii Kang amevunja rekodi hiyo.

Kang alifungua rasmi ukurasa wake wa Instagram siku ya mwaka mpya na kupata watu milioni moja ndani ya saa 11 na dakika 36.

Rekodi ya papa Francis ya saa 12, ilikuwa alipofungua ukurasa wa Vatican Instagram,mwaka 2016.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Papa Francis ana umri wa miaka 82, lakini bado anawasisimua watu wengi kwenye mtandao wa kijamii

David Beckham alipata wafuasi milioni wa Instagram baada ya saa 25 mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kang sasa ana wafuasi milioni 1.4 baada ya kuweka picha saba tu.

Kang yupo katika bendi ya muziki inayoitwa 'Korean boyband' na picha alizoweka kwenye mtandao ni video inayoonyesha akiwa anafanya muziki, Picha alizojipiga mwenyewe na video ya paka wake.

Wakati Kang akiwa ameanza vizuri katika mtandao wa Instagram , ana safari ndefu ya kumpiku mtu kama Cristiano Ronaldo ambaye sasa ana wafuasi zaidi ya milioni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii