Kanisa kubwa zaidi Mashariki ya Kati lafunguliwa Cairo, Misri - Trump afurahia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kanisa hilo jipya linaweza kutoshea watu 8,000

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameongoza ufunguzi wa kanisa jipya la Coptic lililojengwa mashariki ya mji mkuu Misri, Cairo.

Kanisa hilo kuu jipya liliendesha misa yake ya kwanza chini ya ulinzi mkali jumapili ya mkesha wa krismasi ya Coptic.

Siku ya Jumamosi, afisa mmoja wa polisi aliuawa alipokuwa akijaribu kuondoa kilipuzi kilichokuwa kimefichwa kwenye paa la nyumba katika mji wa Nasr viungani mwa mji mkuu wa Cairo.

Waumini wa madhehebu ya Coptic ni 10% ya raia wote nchini Misri ambako idadi kubwa ya watu ni Wislamu.

Wenge wanasema serikali inawabagua na kwamba haiwapatii ulinzi wa kutosha.

Majeshi ya Misri yalitoa ulinzi mkali huku waumini wakipitia sehemu tatu zenye ulinzi kabambe kabla ya kuingia nadni ya kanisa kuu jipya nchini Misri Haki miliki ya picha EPA
Image caption Majeshi ya Misri yalitoa ulinzi mkali huku waumini wakipitia sehemu tatu zenye ulinzi kabambe kabla ya kuingia nadni ya kanisa kuu jipya nchini Misri

Bwana Sisi, ambaye alijitangaza kuwa mlinzi wa wakristo dhidi ya makundi ya watu wenye misimamo mikali, aliliwaambia waumini kuwa ufunguzi wa pamoja wa Kanisa hilo kuu jipya na msikiti wa Al-Fattah Al-Aleem ni ishara ya umoja wao.

"Sisi ni wamoja na tutasalia kuwa pamoja,"Bwana Sisi alisema akifungua kanisa hilo akiashiria waumini wa dini ya Kikristo na Kislam nchini Misri.

Rais wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye Twitter: "Nafurahia sana kuwaona marafiki zetu wa Misri wakifungua kanisa kubwa zaidi Mashariki ya Kati. Rais El-Sisi anaongoza taifa hilo kwenye siku za usoni za kuwajumuisha wote!"

Papa Tawadros II (Kushoto) aliongoza misa misa iliyohudhuriwa na Rais Abdel Fattah al-Sisi (Kulia) Haki miliki ya picha EPA
Image caption Papa Tawadros II (Kushoto) aliongoza misa iliyohudhuriwa na Rais Abdel Fattah al-Sisi (Kulia)
Waumini wakiwa ndani ya kanisa kuu jimpya la coptic ambalo linaweza kuhimili watu 8,000 Haki miliki ya picha AFP/Getty

Papa Francis alitoa salamu za heri njema kwa Papa Tawadros II Alexandria,ambaye ndiye mkuu wa kanisa la Coptic, baadaye aliongoza misa.

PapaTawadros IIaliwaambia waumini kwamba wao ni mashuhuda wa kufunguliwa kwa kanisa kuu Haki miliki ya picha EPA
Image caption PapaTawadros IIaliwaambia waumini kwamba wao ni mashuhuda wa kufunguliwa kwa kanisa kuu
Kanisa kuu jipya la Coptic liko kilo mita 45 mashariki mwa mji wa Cairo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanisa kuu jipya la Coptic liko kilo mita 45 mashariki mwa mji wa Cairo

Msikiti mpya wa Al-Fattah Al-Aleem ni mkubwa mara mbili ya kanisakuu jimpya na mijengo yote ya ibada iko katika mji mkuu wa Misri Cairo

Wafanyikazi wakiendelea na shughuli zao katika msikiti mpya wa Al-Fattah Al-Alim, 45km Mashariki mwa mji wa Cairo Haki miliki ya picha EPA
Wafanyikazi wakiendelea na shughuli zao katika msikiti mpya wa Al-Fattah Al-Alim, 45km Mashariki mwa mji wa Cairo Haki miliki ya picha EPA

Picha zote ziko na haki miliki

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii