Kazakh: Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena, baada ya kufukuliwa miaka 50 iliyopita

The Golden Man armour in the Kazakh National Museum Haki miliki ya picha Kazakh TV
Image caption Binadamu huyo wa dhahabu anaaminika kuwa kiongozi mashuhuri wa vizazi vilivyopita.

Kazakhstan itazika tena mabaki ya mwili wa shujaa wa kipekee katika hifadhi ya kihistoria kwa ajili ya watu wa baadae. Matumaini yao ni kwamba vizazi vya baadae watafanikiwa kugundua asili ya mtu huyo.

Wanahistoria waligundua mabaki hayo yakiwa yamembatana na silaha za dhahabu safi pamoja na sanaa mbali mbali za thamani wakati wakichimba katika makaburi ya Issyk kusini mwa nchi hiyo mwaka 1969, na hapo hapo wakampa jina la "binadamu wa dhahabu".

Tangu uhuru mwaka 1991 amekuwa ni ishara ya urithi wa asili wa taifa huko Kazakhstan. Silaha yake ya dhahabu imekuwa ni kitu cha kujivunia na imehifadhiwa katika hifadhi ya taifa ya Astana, pia hudhuru sehemu mbali mbali duniani kama alama ya tamaduni ya Kazakh.

Haki miliki ya picha Khazakh TV
Image caption Mifupa ya Mtu wa dhahabu imehifadhiwa katika boksi lililo kingwa na karatasi za picha.

Lakini ni machache tu yanajulikana kuhusu shujaa huyo, huku watafiti wakishangazwa na utajiri wa vito vya dhahabu walizo kuta na kwa kiasi kikubwa wakaachana na mabaki ya mtu.

'Pumzika kwa amani'

Mifupa ilipatikana tena hivi karibuni katika taasisi ya upelelezi wa mambo ya kale, yakiwa yamehifadhiwa katika boksi huku yakiambatanishwa na karatasi iliyo andikwa "The Golden Man, May He Rest in Peace", yaani "Binadamu wa dhahabu, apumzike kwa amani."

"Tunajua umri wake na maisha yake ya kijamii, wakati kipimo cha vinasaba kinaweza tupatia taarifa nyingi kupita kiasi," mtafiti Dosym Zikiriya anaiambia Kazakh TV.

Lakini Yermek Zhasybayev wa hifadhi ya Issyk ametoa matumaini kidogo sana juu ya upatikanaji wa taarifa. "Mifupa ipo katika hali mbaya. Imehifadhiwa katika box kwa miaka 50 sasa na imekuwa ikikumbana na kila aina ya kakteria na virusi vikiwemo virusi vya sasa. Kwa sasa ni ngumu kupata taarifa sahihi za vina saba - ila kama tungalikuwa na fuvu au walau jino moja," amekiambia kituo kimoja cha televisheni.

Image caption Umaarufu wa mwanaume wa dhahabu umekuwa sehemu ya urithi wa utamaduni wa Kazakh

Wanasayansi wanasema matumaini yao ni kuhifadhi mabaki katika hifadhi maalumu kwa ajili ya vizazi vijavyo ili kuepuka kuharibika zaidi kwani teknolojia inazidi kukua inaweza waruhusu vizazi vijavyo kupata taarifa nyingi zaidi kuhusu shujaa huyo aliyefariki tangu kale.

"Katika kutambua heshima ya binadamu huyo wa dhahabu, kuzikwa tena kwa mabaki ya shujaa huyo kutaambatana na sherehe za kimila ili kuendana na tamaduni za kifalme za miaka ya nyuma", Kazakh TV imefafanua.

Wanahistoria wanaimani kwamba mabaki hayo ni ya karne ya pili mpaka ya tatu kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, wakati ambao kusini mashariki mwa Kazakhstan ilikuwa ni makazi ya watu wa kabila la Saka, ambao walikuwa wanaaminika kuwa sehemu ya wa Scythian watu wa jamii ya kuhama hama.

Walifukuzwa taratibu baada ya kuwasili mababu wa vizazi vya kale vya Kazakhs Kipchak Turks, lakini wa khazastan hii ya sasa imechukua wasifu wa Binadamu za dhahabu kuwa kiini cha historia yake.

Anaonekana katika maeneo mengi kama alama ya uhuru kote nchini, ikiwa ni pamoja na mji wa Astana na mji maarufu wa biashara wa Almaty ikiwemo pia kwenye maeneo ya Raisi na sarafu ya nchi hiyo.

'Mwanamke wa dhahabu?'

Taarifa za binadamu wa dhahabu zimegusa jicho la watayarishaji vipindi vya BBC ambao walitengeneza makala ya mwaka 2017 iliyotangazwa na mwanahistoria Bettany Hughes.

Lakini inaaminika kuwa vipimo vya vinasaba vya kizazi kijacho huenda vikatatua maswali kama je ni mwanaume wa dhahabu au mwanamke wa dhahabu?

Watafiti wa mambo ya kale wanasema mpaka sasa hakuna uthibitisho kutokana na asili ya utafiti wa mabaki kwani kuna mabaki yaliwahi kupatikana katika mfumo huo ambayo yalikuwa ni ya kaburi la mwanamke kusini mwa Urusi.

Haki miliki ya picha Khazakh TV
Image caption Mabaki machache ya mwanaume wa dhahabu yata zikwa upya mwaka huu