Jeshi la Nigeria lavamia ofisi za gazeti la Daily Trust kwa 'kuhatarisha usalama'

Soldiers by the gate of the Daily Trust newspaper in Abuja, Nigeria Haki miliki ya picha Daily Trust
Image caption Wanajeshi wakionekana katika geti la ofisi za Daily Trust huko Abuja.

Jeshi la Nigeria limesema limevamia ofisi za gazeti la kila siku la Daily Trust kwa kuhatarisha usalama wa nchi baada ya kuripoti kuhusu oparesheni ambazo zimepangwa kutekelezwa na jeshi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

"Makala hiyo inahatarisha waziwazi usalama wa wanajeshi," jeshi limesema katika tamko lililotolewa baada ya uvamizi huo.

Waandishi wawili katika ofisi za gazeti hilo zilizopo kaskazini mashariki katika mji wa Maiduguri wamekamatwa.

Uongozi wa gazeti hilo umelaani kitendo hicho na kutaka wafanyakazi wake waachiwe huru.

Gazeti hilo liliripoti siku ya Jumapili kuwa kuna mpango unasukwa ili kurejesha tena maeneo yaliyo chukuliwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram hivi karibuni yaliyopo kaskazini mashariki mwa mji wa Borno.

Jeshi la Nigeria limesema halijapanga kunyamazisha vyombo vya habari, lakini limelazimika kufanya hivyo kwa sababu gazeti hilo lilitoa taarifa ambazo ni za siri.

"Taarifa hiyo imewapa magaidi wa Boko Haram notisi ya mipango yetu na kuwatahadharishadhidi ya jeshi la Nigeria na kwa namna hiyo kuhujumu mipango ya kijeshi na kuweka maisha ya wanajeshi rehani," taarifa ya jeshi imesisitiza.

'Kompyuta zakamatwa'

Mhariri Mkuu waDaily Trust Mannir Dan-Ali amesema uvamizi wa ofisi za gazeti hilo katika miji ya Maiduguri na mji mkuu wa Abuja umefanyika "kinyume cha sheria".

Wanajeshi walitimua wafanyakazi kutoka ndani ya ofisi hizo na kupora kompyuta kadhaa ambazo waliondoka nazo, amesema Ali katika taarif yake.

ers have been fighting Boko Haram militants since

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na Boko Haram toka 2009

Dan-Ali pia amesema mhariri wa eneo la Uthman Abubakar, pamoja na ripotr Ibrahim Sawab, bado wapo mikononi mwa jeshi.

Wanamgambo wa Boko Haram ambao wamekuwa wakizua ghasia katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria toka 2009, wanapigana ili kuipindua serikali ili kuunda Dola la Kiislamu.

Kwa mujibu wa Daily Trust, ambalo ni moja ya mgazeti makubwa na yanayoheshimika nchini humo, wanajeshi walilazimisha kuingia ndani ya ofisi zao za Abuja wakiwa katika magari matatu yaliyojaza askari.

Wiki iliyopita, mashuhuda waliiambia BBC kuwa wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Islamic State (IS) walisimika bendera yao katika kijiji cha uvuvi cha Baga hali iliyowafanya mamia ya watu kukimbia.

Kundi la IS katika jimbo la Afrika Magharibi ama Iswap, ni kikundi kilichochipuka kutoka Boko Haram hivi karibuni kilidai kuvamia na kuchukua silaha kabla ya kuchoma moto kambi ya jeshi katika upwa wa Ziwa Chad.

Katika habari iliyoandikwa na Daily Trust ilidaiwa kuwa jeshi limejipanga kurudisha katika himaya yake mji wa Baga pamoja na miji ya Doron-Baga, Kross Kawwa, Bunduran, Kekeno na Kukawa ambayo hivi karibuni ilitekwa na Iswap.

Wachambuzi wanadai kuwa jeshi halipendi kukosolewa na mara kadha hukataa kuthibitisha pale wanaposhindwa katika mapambano na wanamgambo hao.

Mwezi Novemba ililichukua jeshi hilo wiki moja kuthibitisha kuwa kambi yake ya Matele kuwa imetekwa na wanamgambo.

Kumekuwa na kuongezeka kasi kwa matukio ya mashambulizi kutoka kwa wanamgambo hao katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi.

Rais Muhammadu Buhari, ambaye anagombea muhula wa pili, aliingia madarakani mwaka 2015 akiahidi kuwasambaratisha wanamgambo hao.

Ingawa jeshi limerudisha maeneo mengi yaliyoshikiliwa hapo awali, bado wanamgambo hao wangali na uwezo wa kutekeleza mashambulizi makubwa.

Mada zinazohusiana