Wataalamu wanapendekeza simu isitumiwe muda mfupi kabla ya kulala

Watoto wanaotumia kompyuta ndogo wakati wa usiku Haki miliki ya picha Getty Images

Kuna ushahidi mdogo kuhusiana na madhara ya utumizi wa vifaa vya kielektroniki kwa watoto, kulingana na muongozo wa afya uliyotolewa na madaktari bingwa wa watoto.

Wazazi hawastahili kuwa na hofu alimradi wamezingatia yaliyomo ndani ya muongozo huo ili kudhibiti muda ambao watoto wao wanatumia kuchezea simu na vifaa vingine vya kielektroniki.

Japo muongozo huo umekwepa kuweka muda maalumu unapendekeza vifaa hivyo visitumiwe muda mfupi kabla ya kulala.

Wataalamu wanasema ni muhimu kuhakikisha utumizi wa vifaa vya kielektroniki hautamzui mtu kupata usingizi, kufanya mazoezi ya viungo au kuathiri utangamano wa familia.

Mengi yaliyoangaziwa katika muongozo huo yametokana na muda wa kutazama televisheni na vifaa vingine vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta.

Chuo cha Royal of Paediatrics (RCPCH), ambacho kinasimamia mafunzo ya wataalamu wa dawa za watoto, imebuni mwongozo wa utumizi wa vifaa hya elektronikii kwa watoto waliyo chini ya umri wa miaka 18.

Muongozo huo umesema hakuna ushahidi wa kutosha ambao unaweza kubainisha kuwa muda mwingi unaotumia simu yako unaweza kuwa na madhara ya kiafya kama inavyodaiwa wakati mwingine..

Uchunguzi zaidi hata hivyo umebaini uhusiano uliyopo kati ya utumizi wa vifaa vya kielektroniki na ongezeko la uzani wa mwili kupita kiasi pamoja na msongo wa mawazo.

Taasisi hiyo ilisema kuwa haitaweka muda wa kudhibiti wakati wa kutumia vifaa hivyo kwa watoto wa umri wowowte kwa sababu hakuna haja ya kufanya hivyo

Badala yake ilishapisha baadhi ya maswali ambayo yatasaidia familia kufanya maamuzi kuhusiana na matumizi yao ya vifaa vya kielektroniki nyumbani:

  • Je familia yako inathibiti muda ambao watu wanatumia vifaa vya kielektroniki?
  • Utumizi wa vifa vya kielektroniki unaathiri kile familia yako inataka kufanya?
  • Je utumizi wa vifaa hiyo hukunyima usingizi?
  • Unaweza kujizuia kula wakati unapotazama televisheni au kutomia simu yako?

Dkt Max Davie, mtaalamu wa afya kutoka taasisi ya RCPCH, anasema utumizi wa kompyuta, simu au vifa vingine vya kielektroniki ni njia bora zaidi ya kufahamu mambo yanayoendelea duniani lakini wazazi wakati mwingine wanaleta dhana kwamba utumizi wake ni mbayo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Anasema: "twataka kubadili msimamo huo na kusema kwamba 'ikiwa majibu yako kwa masuali hayo ni sawa na umeridhika nayo basi unaweza kuendelea mbele na maisha yako bila wasi wasi '.

"Lakini ikiwa majibu yako kwa maswali hayo ni mabaya na wakati mwingine unapata shida kulala basi huenda tatizo hilo linatokana na kuangalia simu au kutazama televisheni kwa muda mrefu ."

Dkt Russell Viner, ambaye ni mkuu wa taasisi ya RCPCH, ameiambia BBC kuwa e "vifa hivyo ni sehemu ya maisha ya kisasa", na kuongeza kuwa : "mambo yamebadilika na hatuna budi kukubali kuwa hatuna uwezo wa kurudi tulikotoka."

Dkt Russell aidha amesema: "Tunahitaji kuwashauri wazazi wajaribu kila wawezalo kusawazisha mambo ili watoto wao wafaidi pande zote mbili .

"Wazazi wanastahili kutafakari ni kitu gani kina umuhimu kwa maisha ya watoto wao."


Wazazi wanasemaje?

Baadhi ya wazazi waliyozungumza na BBC wanasema kuwa hawakubaliani na muongozo huo wa wataalamu kwasababu hawapatia majibu kamili.

"Sina pingamizi kuwa muda mwingi unaotumiwa na watoto kuchezea simu au kitizama televisheni unaathiri masomo yao shuleni na pia kuwafanya wazembe," anasema Andy, ambaye ni mzazi wa kijana wa mika 14.

Andy anasema amemzuia mtoto wake kutumia vifaa hivyo hadi siku ya ijumaa na juma mosi baada ya kutoka shule.

Licha ya mvutano kati yao anasema ameshuhudia kuimarika kwa masomo ya mwanawe.


Wataalamu wanapendekeza nini?

Watoto wasitumia vifaa vya kielektroniki saa chache kabla ya kulala kutokana na ushahidi uliyobainishwa kuwa mwangaza unaotokana na vifaa hivyo huenda ukamyima mtoto usingizi.


Ushauri kwa wazazi:

Haki miliki ya picha Getty Images
  • Wakati wakula chakula ni nafasi nzuri ya kuweka kando simu yako
  • Ikiwa mtoto hataki kuweka kando simu yake wati huo, ipo haja ya wazazi kuingilia kati
  • Wazazi wanatakiwa pia kutafakari muda amabo wao wenyewe wanaotumia simu zao, hasa kama wanafanya hivyo mara kwa mara.
  • Watoto wadogo wanataka mazungumzo ya ana kwa ana badala ya mawasiliano ya mtandaoni

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii