Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 11.01.2019: Higuain, Mata, Sancho, Batshuayi, Heaton, Origi

Gonzalo Higuain Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gonzalo Higuain

Chelsea inapania kumsaini Gonzalo Higuain kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu - japo Juventus ina mpango kumuuza nyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 31. (Telegraph)

Winga wa England Jadon Sancho, 18, ana mpango wa kusalia Borussia Dortmund licha ya tetesi kuwa huenda akarejea katika ligi ya Premia. (Mail)

Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyo ng'ang'ania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Belgium, Michy Batshuayi baada ya mkataba wake wa kuchezea Valencia kwa mkopo kukatizwa. (Telegraph)

Crystal Palace na Fulham pia wanawania kumsaini Batshuayi. (Mirror)

Newcastle imeungana na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Trabzonspor Abdulkadir Omur.

Kiungo huyo wa miaka 19 amebatizwa jina la 'Turkish Lionel Messi'. (Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uhispania Juan Mata, 30, amesema hajui hatima yake ya siku zijazo baada ya kandarasi yake kukamilika mwisho wa msimu huu. (AS - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Juan Mata amefunga mabao 36 katika mechi 146 tangu alipojiunga na Manchester United mwaka 2014

Meneja wa England Gareth Southgate anatafakari kumrudisha kipa wa Burnley Tom Heaton, 32. (Mail)

Wolves wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi mwezi huu wa Januari.

Origi, 23, aliifungia Liverpool bao moja wakati wa mchuano wao wa kombe FA dhidi ya Wolves siku ya Jumatatu. (Birmingham Mail)

Nicolo Barella ambaye anapigiwa upatu kuhamia Stamford Bridge mwezi huu huenda amebadili msimamo.

Haki miliki ya picha SNTV
Image caption Maurizio Sarri(kulia)

Meneja wa klabu hiyo Maurizio Sarri anajiandaa kulipa euro milioni 45 kumnunua kiungo huyo wa kati wa Cagliari kujaza pengo linalitarajiwa kuachwa na Cesc Fabregas. (Tutto Mercato, via Talksport)

Fulham wako katika mazungumzo ya kumsaini beki wa kulia wa Bordeaux na Senegal Youssouf Sabaly, 25. (Sky Sports)

Mneja wa Watford Javi Gracia amesema kuwa hatamsajili mchezaji yeote mwezi msimu huu wa uhamisho. (Independent)

Leicester imekataa dau la Huddersfield la kumnunua mshambuliaji wa Japan Shinji Okazaki, 32. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shinji Okazaki

Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira anatarajiwa kuzungumza na aliyekuwa meneja wa wa Manchester United Jose Mourinho kuhusu uwezekano wa yeye kurudi nyumbani na kuongoza klabu hiyo. (A Bola - in Portuguese)

Hata hivyo, Mourinho amepuuzilia mbali uwezekano wake wa kurudi Ureno. (Correia de Manha - in Portuguese)

Swansea City na Sunderland ni miongoni mwa vilabu vinavyopania kumsajili mshambuliaji wa Ayr United Lawrence Shankland.

Meneja wa klabu hiyo Ian McCall amesisitiza kuwa mkataba wowote utakaofikiwa lazima umshikilie mchezaji huyo kuchezea klabu yoyote ya Uskochi kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Wales Online)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jose Mourinho( kushoto)

Real Madrid pia wanapani kurudisha meneja wao wa zamani, Jose Mourinho katika uga Bernabeu lakini watalazimika kuilipa Manchester United euro milioni 10m ikiwa watamuajiri. (Sun)

Reading huenda wakamsaini kwa mkopo kipa wa Manchester United Joel Pereira, 22.

Pereira anarejea Old Trafford baada ya kuichezea klabu Vitoria Setubal ya Ureno kwa mkopo. (Mail)

Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Hoffenheim na Austria Florian Grillitsch, 23. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alberto Moreno

Beki wa kushoto wa Liverpool na Uhispania Alberto Moreno, 26, amesema kuwa hana mpango wa kuongeza muda mkataba wake katika klabu hiyo itakapomalizika. (Estadio Deportivo - in Spanish)

Mlinzi wa West Ham Reece Oxford, 20, anatarajiwa kushauriana na ajenti wake kuhusiana na hatima yake katika uga wa London Stadium. (Mail)

Chelsea inakaribia kuafikiana na Zenit kuhusiana na mpango wake wa kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes, 24. (Sportitalia, via Metro)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii