Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 13.01.2019: Southgate, Simeone, Kane, Valencia, Fellaini, Tosun, Wilson

Gareth Southgate Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumuajiri meneja wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate huku kampeini ya kumtafuta mrithi wa Jose Mourinho ikiendelea. (Sunday Telegraph)

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unakamilika miezi 18 ijayo pia yuko katika orodha ya meneja mpya wa United. (Sunday Mirror)

Tottenham wameweka euro milioni 310 kuwa bei ya kumnunua mshambuliaji wake Harry Kane huku kukiwa na tetesi kuwa Real Madrid wanamlenga nyota huyo wa miaka 25 (Sun on Sunday)

Arsenal wanaitaka Juventus kulipa euro milioni 18 kumsaini Aaron Ramsey mwezi huu wa Januari ikiwa klabu hiyo ya Italia haitasubiri kandarasi yake ikamilike msimu huu. (Sunday Mirror)

Real Madrid inatarajiwa kuweka dau la kuwanunua mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, pamoja na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 26, msumu wa joto wakati wawili hao watakua wameslia na mwaka mmoja kukamilisha mikataba yao. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eden Hazard

Tottenham wako tayari kufikia ofa ya Paris St-Germain kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong ili achukue nafasi ya Christian Eriksen. (Sunday Express)

West Ham wanatarajiwa kutoa ofa nyingine ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, baada ya ofa yao ya kwanza ya euro milioni 10 kukataliwa. (Sunday Express)

Nahodha wa Manchester United Antonio Valencia, 33, anajianda kuondoka Old Trafford kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu.

Inter Milan wanapigiwa upatu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ecuador. (Sunday Mirror)

AC Milan wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji Marouane Fellaini, 31. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marouane Fellaini

Chelsea wanamfuatilia kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot.

Kiungo huyo wa miaka 23 raia wa Ufaransa pia analengwa na Barcelona. (L'Equipe - in French)

Juventus wamekataa ofa ya Chelsea ya kubadilishana Alvaro Morata na Gonzalo Higuain. (Calciomercato)

Ufungaji mabao wa Mohammed Salah umefikia kiwango cha Harry Kane wa Tottenham na Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal ambaye anaongoza katika chati ya ufungaji mabao katika ligi ya England.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ufungaji mabao wa Mohammed Salah wazidi kuimarika

Ushindi wa Liverpool na West Ham, umewaponza Palace na Leicester

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho ameamua kusalia Barcelona licha ya tetesi kuwa hafurahii uwepo wake Nou Camp.

Manchester United wameonyesha nia ya kumregesha mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool katika ligi ya Primia. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Winga wa Chelsea na Brazil Willian analengwa na klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.

Kiungo huyo wa miaka 30 pia anatafutwa na Barcelona. (Sunday Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Willian(kulia)

Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumsajili Allan, 28 ambaye ni kiungo wa kati wa Napoli na Brazil. (Tuttomercato - in Italian)

Kuna uwezekano wa Arsenal kumpatia Suarez mkataba wa kudumu (Mundo Deportivo - in Spanish)

West Ham huenda wakamnunua mshambuliaji wa Bournemouth na England, Callum Wilson, 26, endapo Marko Arnautovic, 29, atahama klabu hiyo. (Mail on Sunday)

Arsenal wanatarajiwa kukamilisha shughuli ya kumsaini Denis Suarez kutoka Barcelona wiki ijayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Denis Suarez(kati kati)

Kiungo wa kati wa West Ham midfielder Pedro Obiang analengwa na Fiorentina.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Equatorial Guinea aliwahi kuchezea Sampdoria ya Italia. (Mail on Sunday)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Wales Matondo, 18, amekataa ofa ya mkataba mpya. (Sun on Sunday)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii