Uhuru wa wanawake Saudia waendelea kukandamizwa

Picha za Salwa zilizopewa BBC Haki miliki ya picha Salwa
Image caption Salwa, 24, alijitenga na familia yake miezi 8 iliyopita amepata hifadhi Canada
Presentational white space

Kisa cha Rahaf al-Qunun, mwanamke wa Saudia aliyeukana Uislamu kinaendelea kuzua mjadala kuhusu madhila wanayopitia wanawake nchini Saudi Arabia.

Bi Mohammed al-Qunun, 18, ambaye juma lililopita aligonga vichwa vya habari duniani kwa kukimbia familia yake na kisha kujifungia hotelini mjini Bankok ili asirudishwe nyumbani alipewa hadhi ya ukimbizi na Umoja wa Mataifa

Huku mjadala kuhusu hali ya haki za wanawake nchini Saudia ikiwa bado unaendelea mwanamke mwingine aliyetoroka nchi hiyo amepewa hifadhi nchini Canada.

Amesimulia BBC kisa chake.

Salwa, 24, aliyetoroka nyumbani akiwa na dada yake mdogo miezi minane iliyopita anaishi mjini Montreal.

Haya ni maneno yake mwenyewe.

Maandalizi

Tumekuwa tukijiandaa kutoroka kwa karibu miaka sita lakini tulistahili kuwa na pasipoti na kitambulisho cha kitaifa kufanya hivyo.

Nilihitaji idhini ya mlezi wangu kupata stakabadhi hizo. (Wanawake nchini Saudia Arabia wanatakiwa kupata idhini ya kufanya mambo mengi kutoka kwa jamaa zao wa kiume).

Kwa bahati nzuri, mimi nilikua na kitambulisho cha kitaifa kwa sababu familia yangu ilinisaidia kupata wakati nilipokua nasoma chuo kikuu.

Pia nilikua na pasipoti kwasababu nilihitajika kuwa nayo ili niweze kufanya mtihani wa kiingereza miaka miwili iliyopita.

Lakini familia yangu iliinipokonya, kwa hivyo nilihitaji kutafuta mbinu ya kuipata tena.

Niliiba funguo ya nyumba ya ndugu yangu alafu nikaenda kutengenezewa ufunguo mwingine kutokana na huo wake

Sikuweza kutoka nyumbani bila idhini yao, lakini nilijificha na kufanya hivyo wakati wamelala.

Ni hatari sana kawa sababu wangelinishika ningepigw ana kuumizwa vibaya sana.

Nilipopata ufunguo nilifanikiwa kupata pasipoti yangu na ya dadangu mdogo.

Pia niliotea baba alipokua amelala nikaitumia akaunti yake kuingia katika mtandao wa wizara ya mambo ya ndani na kubadilisha namba yake na kuweka ile ya kwangu.

Pia nilitumia akaunti yake kutoa idhini ya kuturuhusu kusafiri nje ya nchi

Jinsi tulivyotoroka

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid

Tuliondoka usiku wa manane wakati kila mmoja nyumbani alikua amelala. Ilikua hali ya kutia hofu sana.

Hatukuweza kuendesha gari kwa hivyo tuliitisha texi. Bahati nzuri karibu kila dereva wa texi Saudia anatokea nchi za kigeni kwa hivyo hawakuona ajabu kutuona tukisafiri peke yetu.

Tulielekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid uliyopo karibu na mji wa Riyadh.

Kama mtu yeyote angelijua kile tulichokua tunafanya nadhani tungeliuawa.

Mwaka wa mwisho wa masomo yangu nilikua nikifanya kazikatika hospitali moja na niliweza kuweka akiba ya kununua tiketi ya ndege na visa ya kupitia Ujerumani.

Pia nilikua napokea pesa zinazotolewa na serikali kwa vijana wasiyokua na kazi kwa hivyo ilinisaidia pakubwa kuweka akiba.

Niliweza kuabuiri ndege ya kwenda Ujerumani na dada yangu.

Ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege na kwa kweli nilikua na furaha isiyokua na kifani.

Nilikua na furaha, nilikua na uoga yani nilikua na hisia ya kila kitu.

Baba yangu alipiga simu polisi alipogundua hatukua nyumbani lakini alikua amechelewa sana.

Kwasababu nilikua nimebadilisha namba yake ya simu katika akaunti yake ya wizara ya mambo ya ndani walipojaribu kumpigia simu walikua wananipigia mimi.

Tulipotoka ndani ya ndege , nilipokea ujumbe wa polisi uliokua umetumiwa baba yangu..

kuwasili

Hakuna maisha Saudi Arabia. Nilikua nikienda chuoni na kurudi nyumba na sikuruhusiwa kufanya kitu kikingine chochote siku nzima.

Walikua wakinikejeli kwa usemi kuwa wanaume pekee ndio wenye uwezo.

Nililazimishwa kusali na kufunga kula.

Nulipofika Ujerumani nilitafuta msaada wa kisheria ili nipewe wakili atakaenisaidia na kutafuta hifadhi.

Nilijaza fomu kadhaa kuelezea kisa changu.

Nilichagua Canada kwasababu ya historia yake nzuri ya kulinda haki za binadamu.

Habari kuhusiana na wakimbizi wa Syria kupewa hifadhi Canada ilinifanya kuvutiwa sana na taifa hilo.

Ndio maana nikaamua hapo ndipo mahali pazuri kwangu kupata hifadhi.

Ombi langu lilikubaliwa na nilipotua Torontoniliona bendera ya Canada katika uwanja wa ndege na nilijivunia sana juhudi zangu.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mimi na dada yangu leo tunaishi Montreal bila hofu yoyote.

Hakuna mtu yeyote hapa anaetulazimisha kufanya lolote.

Huenda Sadia kuna pesa nyingi laki mara mia bora hapa kwa sababu nikitaka kutoka ndani ya nyumba sihitaji kupewa idhini, natoka tu.

Uhuru huo unanifanya kuwa na furaha sana. Najisikia huru kuvalia nguo yoyote ninayoka.

Napendezwa na hali ya hewa hapa....msimu wa joto na hata wakati wa baridi kali nafurahia kuona theluji.

Najifunza lugha ya kifaransa lakini nikigumu sana!

Pia najifundisha kuendesha baisikeli,kuogelea na kuteleza kwenye barafu.

Najihisi kuwa naisha yangu yanaimarika.

Sina mawasiliano na jamaa zangu lakini nadhani ni jambo jema kwetu na kwao pia.

Hapa ni nyumbani na sijutii hatua yangu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii