Waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez ameapa kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake

Maandamano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake Uhispania Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maandamano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake Uhispania

Mwanamume aliyeshtakiwa kwa kumuua mke wake miaka kadhaa iliyopita nchini Uhispania sasa anadaiwa kumuua wakili wake na kisha kujitoa uhai .

Jose Javier Salvador Calvo, 50, aliruka kutoka kwenye daraja la mji wa mashariki wa Teruel polisi walipojaribu kumkamata.

Kisa hicho kimewagutusha watu nchini Uhispania na kuzua mjadala mkali kuhusu sheria ya mzozo wa kinyumbani nchini humo.

Akizungumzia vifo hivyo waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez ameapa kuendeleza juhudi za kukabiliana na visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Tunafahamu nini kufikia sasa?

Jose Javier Salvador Calvo alimpiga risasi na kumuua mke wake, Patricia Maurel Conte, 29, mwezi Mei mwaka 2003 katika eneo la Aragon kaskazini mashariki mwa Uhispani.

Baada ya kuachilia chini ya sheria maalum mwaka 2017, muuaji huyo alijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Rebeca Santamalia Cáncer, 47,wakili aliyemtetea mahakamani aliposhtakiwa kwa mauaji,kwa kujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.

Polisi ilimpata wakili huyoakiwa ameuawa kwa kudungwa kisu katika nyumba ya Salvador Calvo iliyopo eneo la Aragon siku ya ijumaa baada ya mume wake kupiga ripoti kuwa ametoweka.

Muda mfupi kabla ya saa sita usiku mwili wa mshukiwa aliyejirusha kutoka daraja la Teruel, mji uliyopo kilo mita 150 kutoka eneo la tukio, ulipatikana na polisi waliyokuwa kazini.

Mwakilishi wa mamlaka ya mtaa huo Carmen Sánchez amewaambia wanahabari kuwa wakili huyo alikua mhasiriwa wa "unyanyasaji wa kijinsia".

Ukatili dhidi ya wanawake ni mbaya kiasi gani Uhispania?

Katika mtandao wake wa Twitter, waziri mkuu Sánchez amesema kuwa wanawake wanne wameuawa nchini Uhispania siku za hivi karibuni na kwamba ipo haja ya kuingilia kati ''jinamizi'' hilo

Mwaka jana jumla ya wanawake 47 waliuawa kutokana na ukatili wa kijinsia nchini Uhispania, wanne kati yao katika eneo la Aragon.

Mwaka jana mauaji ya mwanamke wa miaka 26 ambaye alivuka mpaka wa Uhispania kutafuta kazi ya uwalimu yalisababisha maandamano makubwa nchini.

Mwoili wake ulipatikana karibu na kijiji cha El Campillo siku tano vaadae.

Mauji ya sasa ya wakili mashuhuri Rebeca Santamalia Cáncer yameibua tena suala la ukatili dhidi ya wananwake Uhispania.

kwa mujibu wa gazeti la El País, mwanamume anaedaiwa kuwa na uhusiano na mwanadada huyo alikiri kumuua baada ya jaribio la kutaka kumbaka kutibuka

Mwanamume huyo kwa jina Bernardo Montoya anaekadiriwa kuwa na miaka 50 aliwahi kufungwa jela kwa kumuua mwanamke mwingine mwaka 1995.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii