Romeo: Chura mpweke ambaye jamii yake imeangamia apata mchumba

Chura mpweke kwa Jina Romeo apata mwenza

Chura anayeaminika kuwa wa mwisho wa aina yake katika ulimwengu ameondolewa upweke.

Romeo, anayejulikana kama chura wa pekee ulimwenguni, ameishi miaka 10 ya kutengwa katika hifadhi ya Bolivia.

Wanasayansi wanasema wamempatia mchumba kwa jina Juliet baada ya safari ya kwenda msitu wa Bolivia.

Chura watano wa majini walipatikana katika vidimbwi vya maji na kukamatwa, kwa kusudi la kuzalishana na kupandikiza upya wanyama hao kwenye pori.

Teresa Camacho Badani ni mkuu wa kitengo cha viumbe hai katika hifadhi asili iliyopo Cochabamba na kiongozi wa safari hiyo.

Anatarajia kwamba vyara hao wa jinsia tofauti watapaendana: "Romeo ni mtulivu na hana mizunguko," aliiambia BBC. "Romeo ana afya na anapenda kula, lakini ana aibu na mpole."

Haki miliki ya picha Robin Moore, Global Wildlife Conservation
Image caption Juliet: Ni Chura jike wa majini

Juliet, hata hivyo, ana utu tofauti sana. "Yeye ana nguvu sana, huogelea sana na anakula sana, wakati mwingine anajaribu kutoroka."

Vyura watano - wanaume watatu na wanawake wawili - ni vyura wa kwanza wa maji kuonekana katika pori kwa miaka kumi, licha ya utafutaji uliofanyika katika jangwa la Bolivia.

Romeo alichukuliwa miaka 10 iliyopita wakati wanabiolojia walipojua aina hiyo ya chura ilikuwa katika shida, lakini hakutarajiwa kubaki peke yake kwa muda mrefu.

Wafanyakazi kulazimishwa wakapumzike Korea Kusini

Alivutia hisia za mataifa mwaka mmoja uliopita juu ya kutafuta kwake mwenzi, na hata alipewa kurasa katika mtandao wa kutafuta mpenzi.

Vyura waliopatikana hivi karibuni wametengwa katika hifadhi ya makumbusho, ambapo huko wanapambana kuhakikisha viumbe hao wanabaki hai.

Haki miliki ya picha Robin Moore, Global Wildlife Conservation
Image caption Juliet akiwa na Teresa Camacho Badani

Chris Jordan kutoka shirika la uhifadhi wa wanyama pori ulimwenguni anasema kuna hatari ya kuwaweka wanyama kama mateka.

Hata hivyo kuna vyura wachache sana porini ambao wanaweza kulinda idadi yao kwa mda mrefu.

"Tuna nafasi halisi ya kuokoa chura wa maji - kurejesha sehemu ya kipekee ya uhai wa misitu ya Bolivia, na kuzalisha taarifa muhimu juu ya jinsi ya kurejesha aina sawa ya vyura hao katika hatari kubwa ya kutoweka."

Haki miliki ya picha Stephane Knoll, Museo de Historia Natural Alcide d
Image caption Vyura wengi wapo katika hatari ya kutoweka

Vyura waliopatikana sasa watatibiwa ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa unaomaliza viumbe hai wengi aina ya amfibia duniani.

Baadae Romeo atakutana na Jullieth, kwa lengo la kujaribu kuzalisha vyura wengine ambao baadae watarejeshwa katika mazingira halisi ya pori.

Nchini Bolivia, asilimia 22 ya aina hii ya amphibian hupata tishio la kuangamia, kutokana na kupoteza makazi, uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa

Haki miliki ya picha Stephane Knoll, Museo de Historia Natural Alcide d
Image caption Utafutaji wa vyura katika vijito vya maji

Teresa Camacho Badani anasema hadithi ya Romeo ni muhimu ili kutoa tahadhari juu ya maafa wanayopata amfibia.

Hawakupata chura wengine wa majini katika mito iliyopo karibu, hii iliibua maswali na wasiwasi juu ya afya ya mazingira.

"Ni fursa nzuri sana kutumia taarifa ya Romeo kusaidia kuelewa vitisho hivi, kusaidia kuelewa jinsi ya kuleta aina hizo kutoka nyuma na pia wakati huo huo kutumia fursa ya kimataifa ambayo Romeo na aina zake wanayo sasa," alisema .

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii