Idadi ya waliyofariki huenda ikaongezeka huku shughuli ya uokozi ikiendelea

Maafisa wa Mexico wakifuatilia moto uliozuka katika bomba la mafuta Haki miliki ya picha Getty Images

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa mlipuko wa bomba la mafuta nchini Mexico, imefikia 66 huku wengine zaidi ya 71 wakijeruhiwa vibaya.

Inaamminiwa kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaushukiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.

Maafisa wanasema mamia ya watu walikua waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuzuka ghafla siku ya Ijumaa.

Picha televisheni zilionesha moto mkubwa na watu waliochomeka vibaya kutokana na moto huo.

Wezi wa mafuta, wanaofahamika kwa jina "huachicoleo" wameongezeka sana katika baadhi ya jamii ya Wamexico.

Miili ilikua imetapakaa katika eneo la tukio baada ya maafisa wa usala kufanikiwa kuuzima moto huo.

Haki miliki ya picha Reuters

Miongo mwa waliyofariki ni mwanamke mmoja na mtoto wa miaka 12, alisema gavana wa jimbo la Hidalgo, Omar Fayad.

Wakaazi waliyojawa na majonzi bado wamefurika eneo la mkasa huo huku maafisa wa wataalamu wa uchunguzi wa maiti wakiendelea kupiga picha mmaiti zilizotapakaa kila mahali.

Serikali imesema wizi wa mafuta umeigharimu taifa hilo karibu dola bilioni tatu mwaka jana.

Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani mwezi Disemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao.

Haki miliki ya picha Reuters

Shirika la mafuta la Pemex, linalomilikiwa na serikali,limesema moto huo ulitokana na mabomba yaliyowekwa kwa njia haramu.

Maelfu ya wanajeshi wamepelekwa katika maeneo tofauti kutoa ulizi wa mabomba ya mafuta katika hatua ambayo imelemaza usafiri maeneo hayo.

Kumeripotiwa uhaba wa mafuta nchini humo huku foleni ndefu zikishuhudiwa katika vituo vya mafuta.

Waziri wa usalama Alfonso Durazo amethibitisha kua moto huo ulizimwa mapema leo asubuhi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa kutoa huduma za dharura wakipelekwa hospitali kwa kutumia helikopta

Gavana wa jimbo la Hidalgo, Omar Fayad, ameonya kuwa idadi ya waliyofariki huenda ikaongezeka huku shughuli ya kuwatafuta waliyochomeka kutokana na mlipuko huo ikiendelea

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa wenyeji walilalazimika kujipatia bidhaa hiyo muhimu kutokana na uhaba wake.

"Watu wengi walifika katika bomba hilo na mitungi yao, kujichotea mafuta kwasababu mafuta yamekua haba sana nchini," mmoja wa wekaazi Martin Trejo aliiambia AFP.

Bwana Martini mwenye umri wa mika 55 alikua katika eneo la mkasa huo kumtafuta mwanawe aliyekua miongoni mwa watu waliokuwa wakichota mafuta.

Baada ya mlipuko huo gavana Fayad, alitoa wito kupitia mtandao wake wa Twitter kuwahimiza watu kuepuka eneo hilo la mkasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Mexico López Obrador amesema kuwa msako dhidi ya wezi wa mafuta umeimarishwa

"Nawaomba mjiepushe na wizi wa mafuta," Bwana Fayad aliandika (kwa lugha ya kihispania). "Kando na kuwa ni uvunjaji wa sheria unahatarisha maisha ya wale wanaohusika.

"Kile kilichofanyika leo Tlahuelilpan haifai kushuhudiwa tena."

Rais López Obrador alifika eneo la mkasa mapema Jumamosi.

Katika mahojiano na vyombo vya habari nchini humo, aliapa kubuni sera kali dhidi ya wezi wa mafuta hadi uhalifu huo utakapotokomwezwa.

"Badala ya kukabiliana na mikasa, tutaimarisha sheria dhidi ya wizi wa mafuta" alisema.

"Jambo la mmsingi kwa sasa nikuwahudumia wale waliojeruhiwa, kuokua maisha, hilo ndilo jambo muhimu."

Hii si mara ya kwanza mkasa wa moto katika bomba la mafuta kutokea Mexico.

Mwaka 2013 watu 37 walifariki dunia baada ya mlipuko kutokea katika makao makuu ya shirika la mafuta la Pemex mjini Mexico City.

Watu wengine 26 wauawa baada ya moto kuzuka katika kiwanda kinngine cha mafuta mwaka 2012.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii