Tazama picha za mwezi mkubwa mwekundu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanzo wa kupatwa kwa mwezi katika mji wa San Diego , California

Wachunguzi wa anga wamekuwa wakitafuta tukio lisilo la kawaida la kupatwa kwa mwezi ambalo lilianza siku ya Jumapili usiku.

Wakati wa tukio hilo mwezi huo unaojulikana kama 'Super Blood Moon', hubadilika na kuwa mwekundu , huku ukionekana kuwa na mwangaza mwingi na ulio karibu na dunia zaidi ya ilivyo siku za kawaida

Tukio hilo lilikuwa likionekana kutoka Kaskazini na marekani kusini, pamoja na magharibi mwa Ulaya. Nchini Uingereza, mawingu mengine yalizuia kuonekana kwa mwezi huo vizuri.

Kupatwa kwa mwezi kunatarajiwa katika kipindi cha miaka miwili, mnamo tarehe 26 mwezi Mei 2021

Walter freeman , naibu profesa katika chuo kikuu cha Syracuse University mjini New York state, alisema: "mwanga mdogo wa jua hutolewa na dunia na kufika katika mwezi, ukijipinda kando kando ya dunia.

Kiwango hiki cha rangi nyekundu huangazia mwezi vya kutosha kwa binadamu kuweza kuona.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kupatwa kwa mwezi kama ilivyokuwa mjini Madrid.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muda mzuri wa mwezi kupatwa ulikuwa mwendo wa 05:12 GMT

Tukio hili hujiri wakati dunia inapopita katikati ya Jua na mwezi.

Katika hali hii, jua huwa nyuma ya dunia huku mwezi ukizunguka katika kivuli cha dunia.

Kupatwa kwa mwezi kulianza mwendo wa 02:35 GMT siku ya Monday na kukamilika saa 07:49 GMT, lakini kipindi ambacho mwezi wote ulikuwa mwekundu ilikuwa mwendo wa 05:12 GMT.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Awamu tofauti za mwezi uliobadilika na kuwa mwekundu mjini Panama

Tukio hilo lisili la kawaida hupata jina 'Super' kutokana na swala kwamba mwezi utakuwa karibu mno na dunia- ambapo utaonekana mkubwa angani zaidi ya ilivyo kawaida.

Nalo Jina "wolf" linatokana na majina yanayopewa miezi mikubwa mwezi Januari "wolf moons".

Haki miliki ya picha PA
Image caption Tukio hilo lilionekana katika mji wa Uingereza wa Liverpool, lakini baadaye ulizimbwa na mawingu.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwezi huo ulionekana mjini Dresden Ujerumani

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii