Ulikua wapi miaka 10 iliyopita? #10YearChallenge yabaini mengi hayajabadilika

Barack Obama akiapishwa kuwa Rais wa Marekani . Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barack Obama akiapishwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Marekani .

Mwaka 2009 Michael Jackson alifariki, Barack Obama aliapishwa kuwa rais wa Marekani na ulimwengu ulikabiliwa na janga la homa ya nguruwe.

Watu kote duniani katika mitandao ya kijamii wamekua wakiweka picha zao za miaka kumi iliyopita wakilinganisha na vile walivyosasa wakitumia hashtag ya 10YearChallenge.

Licha ya baadhi ya watu kuwa na kuhisia wamebadilika "jamani nimezeeka", ukweli ni kwamba mambo mengi duniani hayajabadilika kama wanavyofikiria.

Bado wapo

Endapo watu waliyofariki wangelifufuka bilashaka wangelikutana na nyusu walizofahamu katika ulingo wa siasa wa mataifa mengi duniani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Unaweza kung'amua nyuso hizi? fuatilia ujue ni kina nani chini ya picha hii

Hawa ni viongozi walioponea mapinduzi, waandishi wa katiba, waliobuni miungano ya uongozi na kushindi wa uchaguzi mara ya pili ambao walikua madarakani miaka 10 iliyopita na hadi sasa wangalipo.

Licha ya mabadiliko ya kisiasa duniani bado wanang'angania madaraka katika mataifa yao.

Tofauti na wao, Switzerland imekuwa na maraisi 10 katika kipindi chamuongo mmoja uliyopita.

Hii ni kutokana na katiba yao ambayo inamhitaji rais kuwa madarakani kwa muhula wa mwa mmoja.

Waliyoponea mapinduzi:

Mstari wa juu kutoka kushoto kwenda kulia: Teodoro Obiang Nguema Mbasogo (Equatorial Guinea); Emomalii Rahmon (Tajikistan); Isaias Afwerki (Eritrea); Alexander Lukashenko (Belarus); Faure Gnassingbé (Togo); Angela Merkel (Ujerumani); Ilham Aliyev (Azerbaijan); Pierre Nkurunziza (Burundi); Evo Morales (Bolivia).

Mstari wa kati kutoka kushoto kwenda kulia: Paul Biya (Cameroon); Joseph Kabila (DRC); Benjamin Netanyahu (Israel); Mahmoud Abbas (Palestine); Nursultan Nazarbayev (Kazakhstan); Abdelaziz Bouteflika (Algeria); Paul Kagame (Rwanda); Yoweri Museveni (Uganda); Omar Al-Bashir (Sudan).

Mstari wa chini kutoka kushoto kwenda kulia: Ali Bongo Ondimba (Gabon); Idriss Déby (Chad); Vladimir Putin (Russia); Denis Sassou Nguesso (Congo); Recep Tayyip Erdoğan (Turkey); Ismaïl Omar Guelleh (Djibouti); Bashar Al-Assad (Syria); Gurbanguly Berdimuhamedow (Turkmenistan).

Viwango vya joto

Haki miliki ya picha NASA
Image caption Viwango vya joto duniani vimeendelea kupanda zaidi ya miaka 10 iliyopita

Ulimwengu umeshuhudia ongezeko la viwango vya joto unaochangiwa na shughuli za watu kwa kipindi cha mwango mmoja.

Hata hivyo mambo bado hayajabadilika kama ilivyotarajiwa licha ya mikakati iliyowekwa kukabiliana na hali hiyo.

Athari ya madiliko ya hali ya hewa itawaathiri zaidi watu wanaoishi katika mataifa masikini, lakini kwa miaka 21 viongozi wa ulimwengu wamefikia suluhisho la muda kudhibiti ongezeko la hali ya joto duniani.

Maazimio ya COP24 yaliyofikiwa mwezi Disemba mwaka 2018 ambayo yalitiwa saini nchini Poland ndio mwongozo wa kwanza kwa serikali kuanza mkakati wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu duniani.

Tayari miaka 10imepita na mpaka sasa hatua iliyopigwa haionekani huku ulimwengu ukiendelea kushuhudia joto kali kila uchao.

Mwaka 2009, Shirika la anga za juu Nasa ilesema kuwa kiwango cha joto duniani ni 0.63C zaidi ya viwango vya joto vilivyoshuhudiwa kati ya miaka 1951-1980, na kufikia mwaka 2017 viwango vya joto duniani vilikua vimeongezeka hadi nyuzi joto 0.90.

Bado ni masikini

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pengo kati ya matajiri na masikini linaendelea kupanuka

Kitu kilichobadilika katika mwongo mmoja uliyopita duniani ni kuongezeka kwa makapuni tajiri hususa yale yanayojishughulisha na mafuta na benki.

Gazeti la Financial Times mwaka 2018 lilitoa orodha ya kampuni 500 tajiri zaidi duniani na orodha hiyo iliongozwa na kampuni zinazojishughulisha na masuala ya teknolojia kama vile Apple, Google, Microsoft, Amazon na Tencent.

Kilichosalia kama ilivyokua ni pengo kubwa la utajiri kati ya matajiri na masikini.

Penge hilo limeendelea kuongezeka kutokana na mzozo mkubwa wa kiuchumi uliyoshuhudiwa duniani mwaka 2008.

Ripoti ya uchunguzi iliyochapishwa na bunge la Uingereza kati ya mwaka 2008 na 2017 mali ya watu matajiri zaidi duniani kwa ujumla ilikua 1% na iliongezeka kwa 6% kila mwaka huku mali ya walewaliyo viwango vya chini ambao ni 99% iliongezeka kwa 3% kila mwaka.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa 1% ya watu tajiri zaidi duniani wanaelekea kudhibiti 64% ya utajiri duniani kufikia 2030.

Bado hakuna usawa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harakati za kuleta usawa wa kijinsia duniani bado zinakabiliwa na kibarua kigumu

Licha ya mikakati iliyowekwa kuhamasisha wanawake kuhusu haki zao mwaka 2018, maisha ya kila ya wanawake bado hayajabadilika kwa kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa.

Baadhi ya mambo yamebadilika?

  • Ndio, "Filamu za utupu" hatimae zimetambulika kama hatia kwa mujibu wa sheria za Uingereza.
  • Ndio, Korea Kusini imefunga moja ya mtandao mkubwa ya filamu za ngono unaoangazia picha za wanawake walio nusu uchi ambao wamenaswa na kamera za siri.
  • Ndio, Saudi Arabia imeruhusu wanawake kuenda uwanjani kushabikia michuano ya kandanda na hata baadhi yao kupewa leseni ya kuendesha magari.
  • Ndio, wanawake nchini India hatimae walipata haki ya kuingia katika maeneo kama vile hekalu ambako walikua wamepigwa marufuku.

Hata hivyo bado baadhi ya wanawake wanafariki majumbani mwao kutokana na athari za ukeketaji nchini Nepal na baadhi ya mataifa ya Afrika.

Wasichana bado wanabakwa na magenge ya wabakaji nchini India.

Uavyaji mimba huwafanya wanawake kufungwa jela El Salvador.

Na sehemu hatari zaidi kwa wanawake duniani ni majumbani mwao.

Pengo la ukosefu wa usawa wa kijinsia katika malipo ya ujira kati ya wanawake na wanaume litachukua muda mrefu kujaza.

Kwa mujibu wa takwimu ya baraza la uchumi duniani mwaka jana, itachukua takriban miaka 202 kuziba pengo hilo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii