Vikosi vya usalama Zimbabwe vyatuhumiwa kwa 'kuwatesa' waandamanaji

Maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta mjini Bulawayo. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta

Tume ya kutetea kutetea haki za binadamu nchini Zimbabwe limewatuhumu maafisa wa usalama kwa kutumia "utaratibu wa mateso" kuzima maaandamano.

Ghasia zilizuka zaidi ya wiki moja iliyopita kufuatia hatua ya serikali ya kuongeza bei ya mafuta.

Msemaji wa serikali ametetea msako huo, ameiambia BBC: "Mambo yakiharibika wakati mwingine unahitaji kutumia nguvu kiasi."

Ripoti zimeibuka kuwa wanajeshi wanadai kuwapiga na kuwaumiza watu katika maeneo tofauti ya mji mkuu wa Harare.

Maafisa walionekana wakipiga kundi kubwa la madereva wa mabasi siku ya Jumanne.

Mwandishi wa BBC Andrew Harding alizungumza mmoja kati ya wanaume 30 waliyokamatwa na kupigwa na maafisa wa polisii.

''Kuongezeka kwa hali ya ghasia nchini Zimbabwe kumeibua maswali kuhusu uwezo wa rais Emmerson Mnangagwa kudhibiti majeshi yaliyomweka madarakani miezi 14 iliyopita.'' aliongeza mwandishi wetu.

Rais Mnangagwa ameahidi kuwa visa vya dhulma dhidi ya wanainchi havitakubaliwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Nini kinachodaiwa?

Katika taarifa yake, tume hiyo imesema kuwa karibu watu wanane wameripotiwa kufariki kutoka wiki iliyopita, "hususana kutokana na majeraha ya risasi".

"Maafisaa wa vikosi vya jeshi la Zimbabwe na polisi waliyojihami wamekuwa wakiwatesa watu.

Mateso hayo yaliyopangwa yanalenga wanaume wanaoishi karibu na maeneo yaliyowekwa vizuizi vya barabarani vilivyochomwa na waandamanaji au wezi," ilisema taarifa hiyo.

Tume hiyo iliangazi kwa kina katika ripoti yake jinsi maafisaaa wa usalama walivyokua wakiingia nyumba za watu usiku na kuwapiga wanaume na wavulana wadogo wa hadi miaka 11.

"Hatua ya kupeleka wanajeshi kutuliza maandamano husababisha maafa makubwa na ukiukaji wa haki za binadamu''iliongeza ripoti hiyo

Rais Mnangagwa amesema nini?

Siku ya Jumatatatu Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alilazimika kukatiza ziara yake barani Ulaya na kurejea nyumbani kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Alitarajiwa kuhudhuria kongamano la kimataifa la kiuchumi mjini Davos Uswizi ili kutafuta waekezaji nchini Zimbabwe.

Alipofika mjini Harare, kupitia mtandao wake wa Twitter, alitoa wito kwa pande zinazozona kuungana katika juhudi za kuimarisha uchumi wa taifa uliyozorota.

Katika msururu wa ujumbe wake alisema, ghasia zinazoshuhudiwa na mienendo ya vikosi vya usalam "haifai na kwani inahujumu Zimbabwe mpya", akiongeza: "ikibidu tutachukua hatua."

Maandamano yalianzaje?

Mapema mwezi huu Bw. Mnangagwa alitangaza alitangaza ongezeko kubwa la bei ya mafuta.

Hatua ya kuongezeko la bei za mafuta imesbabisha maandamano ya vurugu katika mji wa kusini magharibu wa Bulawayo.

Raia wengi wa Zimbabwe ambao wamekabilian na hali ngumu ya kiuchumi kwa miaka kadhaa ghafla wamejipata hawawezi kumudu gharama ya usafiri kuenda kazini

Serikali inamlaumu nani?

Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

Msemaji wa rais George Charamba siku ya jumapilialisema: "Uongozi wa MDC wamekuwa wakisema watatumia kila njia ikiwemo maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana."

Upinzani ulipinga uamuzi wa mahakama wa mwezi Agost mwaka jana uliyothibitisha kuwa rais Mnangagwa alimshinda kiongozi wa MDC Nelson Chamisa.

Upinzani umesema nini?

Siku ya Jumanne kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change, Nelson Chamisa alisema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

Chamisa ameiambia BBC kwamba 'hakuna sababu yoyote ile ya wanajeshi kutumia silaha za moto barabarani, kuwapiga raia".

watu wanafuatwa nyumbani kwao, wanatolewa nje na familia zao hata kama wamelala... watu wengi wamekamatwa bila ya sababu ya maana," amesema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii