‘Lady Jay Dee na Erick Winaina na waomboleza kifo cha Mtukudzi’
Huwezi kusikiliza tena

Oliver Mtukudzi amekuwa katika taaluma ya muziki kwa zaidi ya miongo minne

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66.Muziki wake mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith. Kwa mara nyingi ujumbe ndani ya muziki wake ulikuwa ni wa ndani kukwepa mkono wa serikali iliyokuwa haipendelei kukosolewa. Wasanii Lady Jay Dee na Eric Winaina kutoka Tanzania na Kenya wanaelezea jinsi Oliver Mtukudzi alivyochangia tasnia ya muziki barani Afrika.

Mada zinazohusiana