Musa Manzini: mwanamuziki aliyepiga gitaa akifanyiwa upasuaji wa ubongo

Musa Manzini: mwanamuziki aliyepiga gitaa akifanyiwa upasuaji wa ubongo

Wakati mwanamuziki wa Jazz Musa Manzini alipogunduliwa kuwa na uvimbe katika ubongo, madaktari wa upasuaji waliamua kwamba kuna njia moja pekee kufanya upasuaji wa kuutoa uvimbe huo, wakati Musa akiwa macho. Jambo ambalo sio la kawaida Afrika ksuini, wapasuaji kutoka Hosiptali ya Inkosi Albert Luthuli Central walimuamsha baada ya kumpoteza fahamu baada ya kupasua tundu katika fuvu lake la kichwa na wakamuambia apige gitaa wakiendelea na operesheni hiyo.