Matokeo ya Kidato cha Nne: Somo la Hisabati bado kaa la moto kwa wanafunzi Tanzania

elimu tanzania girls Haki miliki ya picha Anthony Asael/Art in All of Us

Mamlaka za mitihani nchini Tanzania zinataka hatua mahususi zichukuliwe katika ufundishaji wa somo la Hisabati na masomo mengine yanayohusisha hesabu.

Matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2018 yametangazwa nchini Tanzania na ufaulu wa masomo hayo bado haujaridhisha.

Ikilinganishwa na mwaka 2017, mwaka jana ufaulu wa masomo hayo umepanda kwa asilimia 0.81.

Mwaka 2017 ufaulu wa Hisabati ulikuwa asilimia 19.19 na mwaka 2018 umefikia asilimia 20. Ufaulu huo ni wa chini kabisa na hafifu mno ikilinganishwa na somo kama Kiswahili ambalo ufaulu wake mwaka 2017 ulikuwa asilimia 84.42 na mwaka 2018 kufikia asilimia 89.32.

Kwa ujumla ufaulu wa masomo yote 2018 ni asilimia 78.37 ambapo ni ongezeko la asilimia 1.28 kutoka asilimia 78.37 ya mwaka 2017.

Gazeti la Mwananchi limemnukuu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) la Tanzania, Dkt Charles Msonde akisema juhudi za makusudi zinahitajika kwa ajili ya kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo yote ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watahiniwa kwenye madaraja ya ufaulu ikiwemo masomo hayo.

Haki miliki ya picha TONY KARUMBA

"Takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi ambao wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza mpaka la tatu wameongezeka kutoka asilimia 27.6 (2016), asilimia 30.15 (2017) na 31.76 (2018)," amesema Msonde na kuongeza, "Matokeo kwa ujumla yanaboreka lakini takwimu zinaonesha wazi kuwa ufaulu wa masomo ya Fizikia, Hisabati na ya Biashara (Commerce na Book-keeping) bado ni duni na wa chini kabisa."

Matokeo yamesalia kuwa chini dhidi ya matarajio ya mtaala kwa somo hilo la hesabati.

Shirika lisilo la serikali Uwezo, linalotathmini viwango vya elimu kwa watoto nchini, katika ripoti yake mnamo 2017 iliyopewa jina 'Are our children learning?' yaani Je watoto wetu wanasoma?Imeeleza kwamba miongoni mwa watoto wa umri ya kati ya miaka 9 hadi 13, wengi hawawezi kukamilisha kazi za kidato cha pili na kuna tofuati kubwa kieneo.

Tofauti hizo zilitaja kwamba zinashinikiza ushawishi mkubwa katika matokeo ya kusoma kuliko masuala mengine kama umaskini na mengineyo yanayohusishwa na ufanisi wa matokeo katika elimu shuleni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii