Bilionea Ken Griffin: Anashikilia rekodi ya kununua majumba ya kifahari katika eneo la Miami

220 Central Park South Haki miliki ya picha Getty Images

Jumba moja la kifahari katika eneo la A Manhattan limeuzwa kwa dola milioni 238 bei ambayo inaifanya kuwa makaazi yaliyouzwa kwa bei ghali zaidi nchini Marekani.

Mali hiyo ni jumba la 220 Central Park South, la ghorofa nne iliyo mkabala na bustani maarufu ya New York park.

Mnunuzi wa mijengo hiyo ya kifahari ni Ken Griffin, mwanzilishi kampuni ya hedge fund Citadel.

BW. Griffin, 50, pia aligonga vichwa vya habari kwa kununua jumba kwa dola milioni 124 karibu na Buckingham Palace mjini London.

Tayari anashikilia rekodi ya kununua majumba ya kifahari katika eneo la Miami, ambayo alinunua kwa dola milioni 60 mwaka 2015, pamoja na Chicago, ambapo alilipa dola milioni 59 mwaka jana.

Bilionea hhuyo pia anamiliki nyumba tatu za kifahari mjini Chicago, sita katika eneo la Florida na mbili mjini Hawaii.

Kabla annue jumba la Central Park, jumba lililokua ghali zaidi nchi Marekani lilikua la East Hampton ambalo liliuzwa kwa kima cha dola milioni 137 mwaka 2014.

Majumba katika eneo la 220 Central Park South yanasemekana kununuliwa haraka licha ya kudorora kwa bei ya makaazi ya kifahari katika soko la New York.

Mwezi Oktoba mwaka jana shirika la Vornado Realty Trust lilifichua kuwa jengo hilo limeuzwa kwa karibu 83%.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ken Griffin amenunua msururu wa makaazi ya kifahari

Tong Tong Zhao, mwanzilishi wa kampuni ya kusimamia mahoteli yenye makao yake mjini Shanghai, amenunua nyumba katika jumba hilo la ghorofa 27 kwa kima cha dola milioni 13.5

Bw. Tong na mke wake Trudie Styler pia wameripotiwa kununua nyumba katika jumba hilo.

Jumba hilo la ghorofa 66 liliundwa na Marekani Robert A M Stern, na lipo katika mtaa unaofahamika kama mtari wa mabilionea.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii