Bwawa la mauti Brazil: Matumaini ya kuwapata manusura yazidi kudidimia

A general view of damage caused by the breakage of a dam containing mineral waste from Vale Haki miliki ya picha EPA

Watu 200 hawajulikani waliko baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil.

Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyikazi wa shirika hilo.

Shughuli ya kuwatafuta manusura inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika jimbo la Minas Gerais.

Gavana wa jimbo hilo Romeu Zema amesema kuna hofu huenda watu wengi wamefariki katika mkasa huo.

Kufikia sasa watu tisa wamethibitishwa kufariki.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Barabara zilizoharibiwa zinatatiza oparesheni ya kuwatafuta manusura

Baadhi ya watu waliyokwama kwenye matope, waliokolewa kwa kutumia helikopta baada ya barabara kuharibiwa.

Watu wengine wamehamishiwa kutoka makaazi yao kutokana na sababu za kiusalama.

Interactive Dam collapse in Brazil

25 January 2019

CBMMG

Earlier this month

Google Maps

Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Vale, Fabio Schvartsman thuluthi moja ya wafanyikazi karibu 300 hawajulikani waliko.

"Nina hofu nataka kujua hali ni mbaya kiasi gani'' alisema Helton Pereira mmoja wa jamaa za watu waliyoathiriwa na mkasa huo aliyezungumza na BBC nje ya hospitali ya Belo Horizonte.

Anasema mke wake na dada yake wote hawajulikani waliko kwa sababu walikuwa wanaendesha biashara ya chakula karibu na eneo la tukio.

Shughuli ya kuwatafuta manusura inafanywa na maafisa 100 wa kukabiliana na hali ya dharura huku wengine zaidi wakitarajiwa kupelekwa katika eneo hilo.

"kuanzia sasa matumaini ya kuwapata waliyohai havuna pengine tutoe miili iliyokwama kwenye matope," alisema gavana Romeu Zema wa jimbo la Minas Gerais.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bwawa hilo linamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Vale, Brazil

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ametaja mkasa huo kama ''janga la kitaifa''.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika "Tunajaribu kila tuwezalo kuwaokoa manusura zaidi wa mkasa huu,".

Maafisa wengine wakuu serikalini wameuru eneo hilo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii